Neno la Leo
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.
Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:14 tunamkuta Daudi bado anakimbia. Sauli hajakata tamaa. Maandiko yanasema alikuwa akimtafuta Daudi kila siku.
Lakini katikati ya simulizi hiyo kuna maneno machache yenye ujumbe mkubwa sana:
“Lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.”
Angalia jambo hilo. Mungu hakumwondoa Sauli mara moja. Hakumaliza tatizo lote siku hiyo. Daudi bado alikuwa jangwani. Bado alikuwa anahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Bado kulikuwa na hatari na uncertainty.
Lakini Mungu alikuwa anamshikilia katikati ya hayo yote.
Mara nyingi tunafikiri ulinzi wa Mungu lazima uonekane kwa tatizo ku...
Muulize Mungu Kabla ya Kuchukua Hatua!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:2 tunamwona Daudi akikabiliwa na uamuzi mwingine muhimu. Anaambiwa kwamba Wafilisti wanashambulia Keila na kuiba mazao yao.
Daudi alikuwa na sababu nyingi za kujiamini. Huyu ndiye aliyemshinda Goliathi. Ana uzoefu wa vita. Sasa ana watu wanaomfuata. Angeweza kusikia taarifa hiyo na kusema, “Hili nalijua. Twendeni kupigana.”
Lakini jambo la kwanza Daudi anafanya linatufundisha kitu muhimu sana:
“Daudi akauliza kwa Bwana.”
Daudi alikuwa na uwezo lakini hakuruhusu uwezo wake uchukue nafasi ya mwongozo wa Mungu.
Na hapo ndipo Neno la leo linapotufikia...
Usihitimishe Hadithi Yako Ukiwa Pangoni!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 22:1–2 tunamkuta Daudi mahali ambapo huenda hakuwahi kufikiria angefika: katika pango la Adulamu.
Fikiria safari yake. Alipakwa mafuta kuwa mfalme. Akamshinda Goliathi. Wanawake wakaimba jina lake. Akaingia katika nyumba ya mfalme na kila kitu kikaonekana kinaelekea juu.
Lakini sasa yuko pangoni.
Kwa macho ya kawaida, unaweza kuangalia maisha ya Daudi na kusema, “Kuna kitu kimeharibika.” Aliyeahidiwa ufalme anawezaje kuwa mkimbizi pangoni?
Lakini Mungu bado hajamaliza.
Akiwa katika pango hilo, watu wanaanza kuja kwa Daudi. Wenye dhiki, wenye madeni na wenye uchungu wa...
Hata Watu wa Imani Huogopa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 21:12–13 tunakutana na upande tofauti kabisa wa Daudi.
Huyu ndiye Daudi aliyesimama mbele ya Goliathi wakati jeshi lote la Israeli limejaa hofu. Huyu ndiye aliyesema, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Huyu ndiye aliyetangaza, “Vita ni vya Bwana.”
Lakini leo Biblia inatuambia kwamba Daudi akaogopa sana.
Akiwa anakimbia kutoka kwa Sauli, anafika Gathi na anapotambua hatari aliyomo, hofu inamjaa kiasi kwamba anajifanya mwendawazimu ili kuokoa maisha yake.
Huyu bado ni Daudi.
Na hilo linatufundisha jambo muhimu sana: kuwa na imani hakumaanishi kwamba hutawahi...
Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia?
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 20:17 tunaendelea kuangalia urafiki wa ajabu kati ya Daudi na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba Yonathani alimpenda Daudi kama alivyoipenda nafsi yake mwenyewe na akamtaka athibitishe tena kiapo chao.
Lakini kuna kitu kinachoufanya urafiki huu kuwa wa kipekee zaidi.
Yonathani alikuwa mwana wa mfalme. Kwa kawaida angeweza kutarajia kwamba siku moja angechukua nafasi ya baba yake. Lakini kadiri Daudi anavyosogea katika kusudi la Mungu juu ya maisha yake, ndivyo uwezekano wa Yonathani kuwa mfalme unavyopungua.
Yonathani angeweza kumwangalia Daudi na kuona competitor. Badala yake, alimwona rafik...
Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 19:4–5 tunamwona Yonathani akifanya jambo linalotuonyesha maana nyingine ya urafiki wa kweli.
Sauli sasa anataka Daudi auawe. Daudi hayupo kwenye mazungumzo haya lakini Yonathani yupo. Na badala ya kukaa kimya, anamkumbusha baba yake ukweli: Daudi hajamkosea. Anamkumbusha jinsi Daudi alivyohatarisha maisha yake kupigana na Goliathi na jinsi Mungu alivyotumia ushindi wake kuleta furaha kwa Israeli.
Lakini kuna jambo kubwa zaidi hapa. Yonathani angeweza kufaidika Daudi akiondolewa. Kama mwana wa Sauli, alikuwa na maslahi yake mwenyewe katika kiti cha enzi. Hata hivyo, Yonathani anachagua kilicho sahihi kuliko kile ki...
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”
Ni rahisi kusimama kwenye sehemu ya kwanza, “Daudi akafanikiwa.” Lakini siri ya maisha yake ipo katika sehemu inayofuata: “Bwana alikuwa pamoja naye.”
Mwezi huu tumemfuata Daudi kutoka malishoni. Tulimwona akiwa kijana asiyepewa nafasi kubwa hata ndani ya familia yake. Akaingia ikulu. Akasimama mbele ya Goliathi. Akapata ushindi na jina lake likaanza kujulikana katika Israeli. Sasa Sauli anaanza kumwonea wivu na kumwangalia kwa mashaka.
<...Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:7–9 tunaona mabadiliko ya kusikitisha yakianza ndani ya moyo wa Sauli. Baada ya ushindi, wanawake wanaimba wakisema Sauli amewaua maelfu yake na Daudi makumi ya maelfu yake. Sauli anasikia comparison hiyo na kuanzia hapo anaanza kumwangalia Daudi kwa jicho tofauti.
Lakini Daudi hajamkosea Sauli. Tatizo ni kwamba mafanikio ya Daudi yameanza kumfanya Sauli ajisikie mdogo.
Na hapo ndipo wivu huanzia mara nyingi. Mtu mwingine anapata promotion na badala ya kufurahi tunaanza kujiuliza, “Kwa nini si mimi?” Biashara yake inakua. Anaolewa au anaoa. Anapata mtoto. Ananunua nyumba. Anapata naf...
Mungu Hutupa Watu wa Kutembea Nasi!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:1–3 tunaanza kuona maisha ya Daudi baada ya ushindi dhidi ya Goliathi. Lakini jambo la kwanza tunalokutana nalo si vita nyingine. Tunakutana na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba moyo wa Yonathani uliungana na moyo wa Daudi, akampenda kama nafsi yake mwenyewe na wakafanya agano la urafiki.
Kwa wakati huu Daudi huenda hajui umuhimu ambao urafiki huu utakuwa nao. Siku zinazokuja hazitakuwa rahisi. Sauli ataanza kumwonea wivu, Daudi atafukuzwa na wakati mwingine maisha yake yatakuwa hatarini. Na katika kipindi hicho, Yonathani atakuwa mmoja wa watu muhimu sana katika maisha yake.
Mu...
Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:49–50 tunafika katika wakati ambao tumekuwa tukiuelekea kwa siku kadhaa. Daudi anaweka mkono katika mfuko wake, anachukua jiwe, analitia katika kombeo na kumpiga Goliathi kwenye paji la uso. Yule mtu aliyekuwa amelitia hofu jeshi zima la Israeli anaanguka.
Goliathi alikuwa na upanga, mkuki, deraya na uzoefu mkubwa wa vita. Daudi alikuwa na kombeo na jiwe.
Lakini tayari tumejifunza kwamba nguvu ya Daudi haikuwa katika jiwe. Tumaini lake lilikuwa kwa Bwana. Hata hivyo, Mungu hakumwambia Daudi atupe kombeo lake. Daudi alimtegemea Mungu huku akitumia kile ambacho tayari alikuwa...
Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.”
Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo lake.
Kwa hiyo kusema “vita ni vya Bwana” hakumaanishi kwamba hatuna sehemu ya kufanya. Inamaanisha tunajua tofauti kati ya wajibu wetu na kile ambacho ni Mungu pekee anaweza kufanya.
Na hapo ndipo Neno la leo linap...
Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.”
Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo lake.
Kwa hiyo kusema “vita ni vya Bwana” hakumaanishi kwamba hatuna sehemu ya kufanya. Inamaanisha tunajua tofauti kati ya wajibu wetu na kile ambacho ni Mungu pekee anaweza kufanya.
Na hapo ndipo Neno la leo linap...
Kwa Jina la Bwana!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa vita na mwonekano wa kutisha. Daudi ana fimbo, kombeo na mawe.
Kwa macho ya kibinadamu, hakuna ushindani.
Lakini Daudi anasema: “Wewe unanijia kwa upanga na fumo na mkuki, bali mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa majeshi.”
Na hapo ndipo tunagundua siri ya ujasiri wa Daudi.
Haikuwa kombeo. Haikuwa jiwe. Wala haikuwa confidence kubwa ndani yake mwen...
Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:38–40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na kumpa upanga. Ni vifaa vizuri kabisa vya vita, lakini Daudi anapojaribu kutembea navyo anatambua jambo muhimu: hajavizoea.
Anavivua.
Badala yake anachukua fimbo yake, mawe matano laini na kombeo lake, vitu ambavyo alikuwa amejifunza kuvitumia muda mrefu akiwa malishoni.
Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila kitu kinachomfaa mtu mwingine kitakufaa wewe. Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu, kupokea ushauri, mentors...
Kumbuka Mungu Alivyokusaidia Zamani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:34–37 tunagundua siri ya ujasiri ambao Daudi alionyesha jana. Sauli anamwangalia Daudi na kuona kijana asiye na uzoefu wa vita. Goliathi, kwa upande mwingine, amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake. Kwa macho ya Sauli, Daudi hana kile kinachohitajika.
Lakini Daudi anajua jambo ambalo Sauli halijui. Ana historia na Mungu.
Anamweleza jinsi alipokuwa akichunga kondoo wa baba yake na simba au dubu akaja kuchukua kondoo, Daudi alimfuata na kumwokoa. Kisha anasema kwa ujasiri: Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba na dubu ataniokoa pia na mkono wa huyu Mf...
Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:32 tunafunga wiki yetu ya kwanza ya Septemba tukiwa tumemfuata Daudi kutoka malishoni mpaka sasa amesimama mbele ya mfalme.
Kwa siku nyingi jeshi la Israeli limekuwa likimsikiliza Goliathi akitoa vitisho. Kila anapotokea, hofu inaenea. Wanaume waliofunzwa vita wanaona ukubwa wa tatizo na mioyo yao inakata tamaa. Lakini Daudi, kijana ambaye hata hakuwa mwanajeshi, anafika mbele ya Sauli na kusema, “Moyo wa mtu yeyote usizimie kwa ajili yake. Mtumishi wako atakwenda kupigana na huyu Mfilisti.”
Mazingira hayajabadilika. Goliathi bado yupo. Jeshi la Wafilisti bado lipo. Kilichobadilika ni kwamba sa...
Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:28–29 tunaendelea na simulizi ya Daudi na Goliathi. Jana tuliona Daudi akiitazama changamoto kwa macho tofauti. Lakini kabla hajafika hata mbele ya Goliathi, anakutana na vita nyingine ambayo huenda hakuitarajia: maneno ya ndugu yake mwenyewe, Eliabu.
Eliabu anamsikia Daudi akiuliza kuhusu Goliathi, anakasirika na kuanza kumshutumu. Anahoji sababu ya Daudi kuja vitani na hata kutafsiri vibaya nia ya moyo wake.
Fikiria hilo: Daudi hajapigana na Goliathi lakini tayari kuna mtu anayemwambia, kwa namna fulani, “Wewe unafanya nini hapa?”
Na maisha yanaweza kuwa hivyo pia. Kabla hujaf...
Usimfanye Goliathi Wako Kuwa Mkubwa Kuliko Mungu
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:26 tunaingia katika moja ya simulizi zinazojulikana zaidi katika Biblia, simulizi ya Daudi na Goliathi. Lakini kabla Daudi hajachukua jiwe, kabla hajatumia kombeo na kabla Goliathi hajaanguka, kuna jambo muhimu sana linalotokea: Daudi anaiona hali ileile ambayo kila mtu anaiona lakini anaichukulia kwa mtazamo tofauti.
Jeshi lote la Israeli lilimwona Goliathi. Waliona ukubwa wake, silaha zake na hatari aliyokuwa nayo. Daudi naye aliona mambo hayo. Imani yake haikumfanya ajifanye kwamba Goliathi hayupo au kwamba si hatari.
Tofauti ilikuwa hii: wengine walimwangalia Goliathi wakajilinganisha naye. Daudi alimwangalia Golia...
Mungu Akifungua Mlango, Atakukuta Uko Tayari?
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 16:18 tunaendelea na simulizi ya Daudi. Jana tulimwona akipakwa mafuta lakini bado hakwenda moja kwa moja kuwa mfalme. Leo tunasikia mtu akimwelezea kwa Sauli: Daudi anajua kupiga kinubi, ni shujaa, ana busara katika kusema na zaidi ya yote, Bwana yu pamoja naye.
Jambo la kuvutia ni kwamba sifa hizi hazikuanza kujengwa siku ambayo nafasi ya kwenda ikulu ilifunguka. Daudi alikuwa ameanza kujiandaa wakati hakuna aliyekuwa akimtazama.
Alijifunza kupiga kinubi bila kujua kwamba siku moja muziki huo ungemfungulia mlango wa ikulu. Alijifunza kuwa mwaminifu akichunga kondoo bila kujua...
Ruhusu Mungu Akutengeneze.
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 16:13 tunaendelea na simulizi ya Daudi. Jana tulimwacha malishoni, mahali ambapo watu hawakumfikiria lakini Mungu alikuwa amemwona. Leo anaitwa nyumbani na Mungu anamwambia Samweli, “Ondoka, umtie mafuta, maana huyu ndiye.” Daudi anapakwa mafuta katikati ya ndugu zake na Roho wa Bwana anakuja juu yake.
Lakini jambo la kushangaza ni hili: Daudi alipakwa mafuta kuwa mfalme lakini hakwenda moja kwa moja kukalia kiti cha enzi.
Alikuwa amechaguliwa lakini bado alikuwa na safari. Kulikuwa na tofauti kati ya kusudi alilopewa na utayari wa kulibeba.
Nasi tunaweza kufanya k...
Usidharau Mahali Ulipo Sasa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 16:11 tunaendelea na safari tuliyoanza jana. Samweli amefika nyumbani kwa Yese kumpaka mafuta mfalme mpya wa Israeli. Wana wa Yese wanapita mbele yake mmoja baada ya mwingine lakini Mungu hamchagui hata mmoja. Hatimaye Samweli anauliza, “Je, hawa ndio wanao wote?”
Ndipo tunagundua kwamba kuna mmoja ambaye hata hakuitwa. Daudi yuko malishoni akichunga kondoo.
Fikiria hilo. Mfalme ajaye wa Israeli yuko shambani wakati mkutano unaohusu maisha yake unaendelea nyumbani. Hakualikwa, hakutajwa mwanzo na hakuna aliyedhani kwamba ndiye ambaye Mungu alikuwa akimtafuta. Lakini kutokualikwa na watu hakumaanishi alikuwa amesahaul...
Mungu Haangalii Sura, Anaangalia Moyo Wako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 16:7 tunaanza mwezi mpya na hatua mpya katika simulizi ya 1 Samweli. Agosti tuliimaliza na Sauli, mtu aliyeanza vizuri lakini ambaye hatua kwa hatua alianza kuweka maamuzi yake mbele ya utiifu kwa Mungu. Sasa Samweli ametumwa nyumbani kwa Yese kumtafuta mfalme mwingine.
Anapomwona Eliabu, Samweli anavutiwa na kile kinachoonekana kwa macho. Anaonekana kama mtu anayefaa kuwa mfalme. Lakini Mungu anamfundisha jambo ambalo litakuwa msingi wa safari yetu na Daudi: mwanadamu huangalia sura ya nje lakini Bwana huangalia moyo.
Na hapo ndipo tunapoanzia Septemba: moyoni.
Tunaishi katik...
Kuanza Vizuri Haitoshi, Linda Imani Yako Mpaka Mwisho!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 15:35 tunafunga safari yetu ya mwezi wa Agosti katika sehemu yenye huzuni. Samweli anamwombolezea Sauli na tunaona huzuni iliyotokana na mwelekeo ambao maisha ya Sauli yalikuwa yamechukua. Ni mwisho mzito lakini wenye somo muhimu sana: si muhimu tu kuanza vizuri, ni muhimu kuendelea kutembea na Mungu.
Tulianza mwezi huu na Hana, mwanamke aliyefika mbele za Mungu akiwa na maumivu, akamimina moyo wake kwake na kujifunza kusubiri. Tukaona Mungu akimjibu na kupitia Samweli tukajifunza kusikiliza sauti ya Mungu, kumtii, kukumbuka Ebenezeri zetu na kuendelea kuwa waaminifu.
Kisha tukam...
Utii ni Bora Kuliko Dhabihu!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 15:22–23 tunafika katika moja ya nyakati muhimu sana katika maisha ya Sauli. Mungu alikuwa amempa agizo lakini Sauli hakulitekeleza kikamilifu. Alipoulizwa kwa nini, akatoa sababu iliyosikika ya kiroho: baadhi ya vitu vilihifadhiwa ili vitolewe sadaka kwa Bwana. Ndipo Samweli akasema maneno ambayo yameendelea kutukumbusha mpaka leo: “Kutii ni bora kuliko dhabihu.”
Tatizo la Sauli halikuwa kwamba hakumtii Mungu kabisa. Alitii sehemu ya agizo na akaacha sehemu ambayo haikumfaa. Kisha akajaribu kutumia jambo la kidini kuhalalisha kile ambacho Mungu hakumwagiza.
Na hapo ndipo Neno la leo linapotufikia sisi pia. J...
Mungu Hahitaji Wengi Ili Kufanya Makubwa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 14:6 tunamwona Yonathani akiwa na mchukua silaha wake wakikabiliana na mazingira ambayo kwa macho ya kibinadamu yanaonekana hayawezekani. Ni watu wawili tu dhidi ya jeshi kubwa la Wafilisti. Lakini Yonathani anatamka ukweli wenye nguvu: “Hakuna kinachoweza kumzuia Bwana kuokoa kwa wengi au kwa wachache.”
Neno la leo linatukumbusha kwamba mara nyingi tunapima uwezekano wa mafanikio kwa kile tulichonacho. Tunaangalia fedha zetu, watu tulio nao, uzoefu wetu, elimu yetu au ukubwa wa nafasi tuliyopewa na kusema, “Hiki hakitoshi.” Lakini kile ambacho hakitoshi mikononi mwetu kinaweza kuwa zaidi ya kutosha kinapowekwa m...
Je, Unaweza Kumsubiri Mungu Wakati Kila Kitu Kinaenda Vibaya?
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 13:13–14 tunaanza kuona ufa mkubwa katika uongozi wa Sauli. Wafilisti wanatishia Israeli, watu wanaanza kutawanyika na Samweli haonekani kufika kwa wakati ambao Sauli alitarajia. Akiwa chini ya presha, Sauli anaamua kuchukua hatua mwenyewe. Tatizo halikuwa kwamba hakufanya chochote. Tatizo ni kwamba alifanya jambo ambalo Mungu hakumwagiza kwa sababu hakuweza kusubiri.
Neno la leo linatukumbusha kwamba wakati mwingine presha ndiyo hufunua kina cha utiifu wetu. Ni rahisi kusubiri wakati kila kitu kiko sawa. Lakini je, tunaweza kuendelea kumtii Mungu wakati muda unaonekana kuisha, watu wanaondoka na mazingira yanatuambia, “Fanya kitu sasa...
Kuna Watu Huwezi Kuwabadilisha, Lakini Unaweza Kuwaombea!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 12:23–24 tunasikia kauli nzito kutoka kwa Samweli: “Hasha kwangu nimtendee Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi.” Hawa ndio watu waliokuwa wamesisitiza kupata mfalme licha ya maonyo waliyopewa. Samweli hakukubaliana na uchaguzi wao lakini hakuruhusu kukatishwa tamaa kwake kugeuke sababu ya kuwaacha.
Neno la leo linatufundisha kwamba upendo wa kweli hauishii pale watu wanapofanya maamuzi tusiyokubaliana nayo. Kuna wakati tunaweza kushauri, kuonya na kuelekeza lakini mtu akaendelea kuchagua njia yake. Tunapofika hapo tunaweza kushindwa kumbadilisha kwa maneno lakini bado tunaweza kumpeleka mbele za Mungu kwa maombi.
Na hapa ndipo...
Je, Utiifu Wako Utastahimili Mafanikio?
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 12:14–15 tunakutana na Israeli katika hatua mpya. Wamepata kile walichosisitiza kukitaka, sasa wana mfalme. Lakini Samweli anawakumbusha kwamba mazingira yao mapya hayajabadilisha jambo la msingi: bado wanapaswa kumcha Bwana, kumtumikia na kuitii sauti yake.
Neno la leo linatufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi hatujiulizi: Je, utiifu wetu kwa Mungu unaweza kustahimili mafanikio? Ni rahisi kumtafuta Mungu tunapohitaji kazi, tunapotafuta mwenza, tunapoanzisha biashara au tunaposubiri mlango fulani ufunguke. Lakini nini kinatokea baada ya kupata kile tulichokuwa tunakiombea? Je, bado tunaomba? Bado tunasikiliza? Bado tunamtii Mungu?
Israeli walikuwa wameing...
Mungu Akikuinua, Usilipize Kisasi kwa Waliokudharau
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 11:13 tunamwona Sauli baada ya kuiongoza Israeli katika ushindi mkubwa. Wale waliowahi kumdharau sasa wako katika nafasi dhaifu na baadhi ya watu wanataka wauawe. Sauli angeweza kutumia wakati huo kulipiza kisasi na kuwanyamazisha wote waliowahi kumtilia shaka. Lakini anakataa na kuelekeza utukufu kwa Mungu: “Kwa maana leo Bwana ametenda wokovu katika Israeli.”
Neno la leo linatufundisha kwamba wakati mwingine tabia yetu haijaribiwi tunapokuwa chini bali tunapofika juu. Ni rahisi kusema tumesamehe wakati hatuna uwezo wa kufanya chochote. Lakini nini kinatokea Mungu anapokupa nafasi, mamlaka au mafanikio na wale waliokudh...
Usiifiche Karama Ambayo Mungu Ameweka Ndani Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 10:22 tunakutana na picha ya kushangaza. Wakati umefika wa Sauli kutangazwa mbele ya watu kama mfalme lakini Sauli haonekani. Wanapomtafuta, Mungu anawaonyesha kwamba amejificha miongoni mwa mizigo. Jana tuliona Roho wa Bwana akimjia Sauli na Mungu akimwezesha kwa ajili ya jukumu lililokuwa mbele yake. Leo mtu yule yule ambaye Mungu amemwandaa anajificha.
Neno la leo linatufanya tujiulize: Kwa nini wakati mwingine tunakimbia kile ambacho Mungu mwenyewe ameweka ndani yetu? Mungu anaweza kutupa karama, uwezo, nafasi au jukumu lakini hofu, kujiona hatutoshi au kuogopa maoni ya watu kukatufanya tujifiche. Kuna...
Mungu Hakuiti Bila Kukupa Uwezo!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 10:6 tunamwona Sauli akikabiliwa na jambo kubwa kuliko maisha aliyokuwa ameyazoea. Mungu alikuwa anamwita kwenye jukumu jipya lakini hakutarajia Sauli alibebe kwa nguvu zake mwenyewe. Samweli anamwambia, “Roho wa Bwana atakujilia kwa nguvu” na kwamba Sauli atabadilishwa kuwa mtu mwingine. Mungu aliyemwita alikuwa pia anaenda kumwandaa na kumwezesha.
Neno la leo linatukumbusha kwamba wakati mwingine Mungu anaweza kutupeleka kwenye majukumu yanayotufanya tujiulize, “Mimi nitawezaje?” Tunaweza kuangalia uwezo wetu, uzoefu wetu au mapungufu yetu na kujiona hatutoshi. Lakini wito wa Mungu hautegemei uwezo wetu pekee. Mungu anapokuita, anakupa pia neema na nguv...
Mungu Ameshaandaa Jibu la Kesho Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 9:16 tunaona jambo ambalo Sauli mwenyewe hakulijua. Wakati bado yuko njiani akitafuta punda wa baba yake, Mungu tayari amezungumza na Samweli kuhusu ujio wake. Sauli alikuwa anaelekea kwenye kesho yake bila kujua kwamba Mungu alikuwa tayari ametangulia mbele yake.
Neno la leo linatukumbusha kwamba tunaweza kuwa na maswali mengi kuhusu kesho, lakini Mungu haingii kesho pamoja nasi kwa mara ya kwanza. Anaijua tayari. Anaweza kuwa anatengeneza mazingira, anaandaa watu na kufungua njia ambazo sisi bado hatuzioni. Hii haimaanishi kwamba kila tunachotamani lazima kitokee kwa namna tunayotaka. Inamaanisha kwamba tunaw...
Kile Ulichopoteza Kinaweza Kukupeleka Kwenye Kusudi Lako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 9:6 tunaanza safari ya Sauli kwa tukio linaloonekana la kawaida kabisa. Punda wa baba yake wamepotea na Sauli anaondoka kwenda kuwatafuta. Lakini kile ambacho Sauli hajui ni kwamba wakati yeye anatafuta punda, Mungu anamwelekeza kuelekea kukutana na Samweli na kwenye hatua ambayo itabadilisha maisha yake kabisa.
Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila safari tunayopitia tutaielewa tunapoianza. Wakati mwingine tunadhani tunatafuta kitu kimoja kumbe Mungu anatumia safari hiyo kutupeleka kwenye jambo ambalo hatukulitarajia. Hata usumbufu, kuchelewa au jambo ambalo halikuwa katika mipango yetu linaweza kuwa sehemu ya njia ambay...
Usipuuze Maonyo ya Mungu Kwa Sababu Tu Hayafanani na Matamanio Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 8:18–19 tunaendelea kuona hatari ya kutamani jambo mpaka tusitake tena kusikia kile Mungu anachosema. Samweli amewaeleza Waisraeli wazi gharama ya kuwa na mfalme lakini pamoja na maonyo hayo wanajibu, “Hapana! Tunataka mfalme juu yetu.” Tatizo halikuwa kwamba Mungu hakuwapa mwongozo. Tatizo ni kwamba tayari walikuwa wameamua jibu walilotaka.
Nasi tunaweza kufanya vivyo hivyo. Tunaweza kuomba, “Bwana uniongoze,” lakini moyoni tayari tumeamua tunakotaka kwenda. Tunaweza kutafuta ushauri mpaka tupate mtu atakayetuambia kile tunachotaka kusikia. Neno la leo linatukumbusha kwamba maonyo ya Mungu pia ni sehemu ya upendo wake. Si kila mlango uli...
Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 8:6–7 tunafika katika hatua muhimu katika historia ya Israeli. Waisraeli wanamtaka mfalme ili wawe “kama mataifa mengine.” Samweli anahuzunika lakini Mungu anamfunulia tatizo kubwa zaidi: “Si wewe waliyekukataa bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.” Walikuwa na Mungu akiwaongoza lakini wakaanza kutamani mfumo waliouona kwa wengine. Neno la leo linatufanya tujiulize kama nasi wakati mwingine tunatamani vitu si kwa sababu tunavihitaji au ni mapenzi ya Mungu bali kwa sababu tunaona wengine wanavyo. Tunaweza kutamani kazi, fedha, mahusiano, nafasi au maisha ya mtu mwingine mpaka tukashindwa kuona kile ambacho Mungu tayari ametupa. Si kila tunacho...
Si Kila Siku Ni Muujiza, Lakini Kila Siku Inahitaji Uaminifu
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 7:15–17 tunamwona Samweli baada ya ushindi mkubwa wa Israeli dhidi ya Wafilisti. Ameweka jiwe la Ebenezeri na kukumbuka msaada wa Mungu lakini hakubaki akiishi katika ushindi wa jana. Biblia inasema aliendelea kuhukumu Israeli siku zote za maisha yake na kila mwaka alizunguka maeneo mbalimbali akitekeleza wajibu wake. Hapa tunajifunza upande muhimu wa maisha ya imani ambao mara nyingi haupati shangwe nyingi: uaminifu wa kila siku. Si kila siku tutashuhudia muujiza mkubwa au kuwa na ushuhuda wa kusisimua. Kuna siku Mungu anatutaka tuamke, tufanye kazi yetu vizuri, tutunze familia zetu, tutimize ahadi z...
Hata Sasa Bwana Ametusaidia!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 7:12 tunafika katika wakati wa ushindi baada ya Israeli kumrudia Mungu. Samweli anasimamisha jiwe na kuliita Ebeneza, akisema, “Hata hapa Bwana ametusaidia.” Jiwe hilo lilikuwa ukumbusho kwamba hawakufika pale kwa nguvu zao wenyewe bali kwa msaada wa Mungu. Nasi tunapoitazama safari ya maisha yetu kuna milima tuliyodhani hatutaivuka, milango tuliyodhani haitafunguka na nyakati ambazo hatukujua tutafikaje kesho. Lakini leo tupo hapa. Neno la leo linatufundisha umuhimu wa kukumbuka uaminifu wa Mungu kwa sababu kumbukumbu ya kile Mungu alichotenda jana hutupa imani ya kumwamini kwa yale yaliyo mbele yetu. Je, unapoitazama safari ya...
Huwezi Kumtumikia Mungu kwa Moyo Uliogawanyika!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 7:3 tunamwona Samweli akiwaita Waisraeli warudi kwa Mungu baada ya miaka ya kupotea. Lakini kurudi kwao hakukuwa suala la kusema tu kwamba wametubu. Samweli aliwataka waondoe miungu mingine na wamwelekee Bwana kwa mioyo yao yote. Neno la leo linatufundisha kwamba toba ya kweli si majuto pekee, lazima ionekane katika mabadiliko ya maisha. Huenda sisi hatuna sanamu kama za Israeli lakini fedha, kazi, mahusiano, tamaa, kutafuta sifa za watu au hata nafsi zetu zinaweza kuchukua nafasi ambayo Mungu pekee anastahili. Je, kuna kitu tunachomwomba Mungu atusamehe lakini bado hatuko tayari kukiacha? Kurud...
Usimzoee Mungu Mpaka Ukasahau Utakatifu Wake!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 6:20 tunakutana na swali zito: “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu?” Baada ya kuona jinsi Mungu alivyoonyesha nguvu zake dhidi ya Wafilisti, sasa Waisraeli wanakumbushwa kwamba Mungu si mwenye nguvu tu, Yeye ni mtakatifu. Neno la leo linatukumbusha kwamba tunaweza kumzoea Mungu kiasi cha kupoteza kicho na heshima tunayopaswa kuwa nayo mbele zake. Ni kweli Mungu ni Baba yetu na anatupenda lakini neema yake haijafanya dhambi kuwa jambo dogo wala utakatifu wake kupungua. Je, ukaribu wetu na Mungu umetufanya tumheshimu zaidi au tumemzoea kiasi kwamba mambo yake mata...
Israeli Walishindwa, Lakini Mungu Hakushindwa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 5:3–4 tunaendelea na simulizi ya Sanduku la Agano baada ya kutekwa na Wafilisti. Wanalichukua na kuliweka katika hekalu la Dagoni kana kwamba ushindi wao dhidi ya Israeli ulimaanisha kuwa mungu wao alikuwa amemshinda Mungu wa Israeli. Lakini asubuhi Dagoni anakutwa ameanguka chini mbele ya Sanduku. Wanamwinua na siku inayofuata anaanguka tena, safari hii kichwa na mikono yake ikiwa imekatwa. Ujumbe ni mzito: Israeli walikuwa wameshindwa vita lakini Mungu wao hakuwa ameshindwa. Neno la leo linatukumbusha kwamba hata tunapopitia kushindwa, kupoteza au mazingira yanayoonekana kuwa nje ya uwezo wetu, tusifikiri kwamba Mungu a...