Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
17 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inakupeleka Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania kumulika uchakataji wa samaki na dagaa bila kutumia kuni. Lengo ni kulinda mazingira kwa kuepusha ukataji wa miti halikadhalika afya za wachakataji.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, kupitia FISH4ACP ambao ni mpango wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibea na Pasifiki unaolenga kuboresha uzalishaji, ushindani na uendelevu wa minyororo ya thamani ya uvuvi na ufugaji wa viumbe vya majini kwenye maeneo hayo, limeendelea kulinda mazingira na kuinua vipato vya jamii
Pia tunakuletea muhtasari wa h...
16 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia silaha za vita zinazojiendesha zenyewe, pamoja na muhtasari wa habari za masuala ya amani na haki za kibinadamu kwa wakimbizi.
Huko Manila, Ufilipino Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amehutubia mkutano wa 16 wa pamoja wa nchi za Jumuiya ya Kusini – Mashariki mwa Asia na Umoja wa Mataifa na kutaka mageuzi ya taasisi za kimataifa ili kutoa nafasi na uwakilishi unaostahili kwa mataifa yanayoinukia kiuchumi na kisiasa, akisema mfumo wa sasa hauakisi hali halisi ya dunia inayozidi kuwa na vituo vingi vya mamlaka.Kitendo cha kupunguzwa kwa kiasi kik...Migogoro na milipuko ya magonjwa DRC yazidisha janga la njaa, watu milioni 30.3 hatarini
Kwa mujibu wa Mfumo wa Umoja wa Umoja wa Mataifa wa tathimini ya viwango vya uhakika wa chakula IPC, hali ya uhaba mkubwa wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), watu milioni 30.3 wakitarajiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wa viwango vya janga au hali mbaya zaidi kati ya mwezi Januari na Juni 2027. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hii na anaeleza kwa kina. Kwako Anold
13 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula nchini DRC, kilmo na mbegu bora nchin Zimbabwe, na biashara ndogondogo na ufugaji kuku kwa wanawake wenye ulemavu nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Mfumo wa Umoja wa Umoja wa Mataifa wa tathimini ya viwango vya uhakika wa chakula IPC, hali ya uhaba mkubwa wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), watu milioni 30.3 wakitarajiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wa viwango vya janga au hali mbaya zaidi kati ya mwezi Januari na Juni 2027. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hii na anaeleza kwa kinaNchini Kenya, Pikoti Chepkemoi, mwanamke mw...Kuwa na ulemavu hakujazima ndoto yangu ya ujasiriamali - Pikoti Chepkemoi
Nchini Kenya, Pikoti Chepkemoi, mwanamke mwenye ulemavu wa miguu kutoka Kaunti ya Pokot Magharibi, ameweza kujikwamua kiuchumi licha ya kuwa na changamoto za ulemavu huo tangu utotoni. Kupitia mafunzo ya ufugaji wa kuku na biashara ndogondogo yanayoambatana na ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake, UN Women ndoto yake imetia. Cynthia Akhangwa na anatujuza zaidi
FAO yawasaidia wakulima nchini Zimbabwe kukabiliana na ukame na kulinda mifugo
Nchini Zimbabwe, ambako ukame unaathiri uzalishaji wa chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, linawasaidia wakulima kutumia mbinu za kuhifadhi maji, kuboresha ufugaji na kutunza mbegu za asili. Kupitia ushirikiano na serikali ya nchi hiyo kuanzia mwaka 2022 hadi mwaka huu 2026, wakulima wamepata mbinu za kuimarisha uzalishaji licha ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
12 NOVEMBA 2026
Leo Novemba 12 mwaka 2026, serikali ya Kenya inaanza kuhesabu siku 42 za kufuatilia iwapo kutaibuka tena maambukizi ya Ebola. Hii ni baada ya mgonjwa wa mwisho wa Ebola aliyekuwa anapatiwa matibabu kupona. Yeye ni miongoni mwa wagonjwa 9 walioambukizwa Ebola ya Bundibugyo tangu iripotiwe nchini humo Oktoba 5 baada ya mgonjwa wa Ebola kuingia Kenya kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) kupitia Uganda. Wagonjwa wawili walifariki dunia na 7 wamepona. Wengi hujiuliza wametibiwa na nini? Assumpta Massoi amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Umma nchini Kenya ambaye anaanza kwa kujitambulisha.
Vijana wasiachwe nyuma - Sara Pima
Tunasalia huko huko Antalya Uturuki kwenye COP31 ambako Sara Pima kutoka Tanzania. Yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi akiwakilisha Afrika, lakini pia yuko kwenye majadiliano kuhusu masuala ya jinsia na kujengea uwezo. Hapa anazungumzia kile wanachopatia kipaumbele katika mkutano huo.
Matumizi ya nishati safi ni kiashiria cha mafanikio ya hatua kwa tabianchi - Guterres
Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika matumizi ya nishati safi duniani yanaonesha kuwa mabadiliko ya haraka kuelekea uchumi usiotegemea nishati za kisukuku yanawezekana, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, hii leo huko Antalya Uturuki hii leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi unaofanyika kwenye Mkutano wa 31 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP31. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
11 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia juhudu za kukabiliana na mabadliko ya tabianchi, na mazishi salama ya miili ya waathirika wa Ebola nchini DRC.
Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika matumizi ya nishati safi duniani yanaonesha kuwa mabadiliko ya haraka kuelekea uchumi usiotegemea nishati za kisukuku yanawezekana, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, hii leo huko Antalya Uturuki hii leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi unaofanyika kwenye Mkutano wa 31 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP31Tunasalia huko huko Antalya Uturuki kwenye COP31 ambako Sara Pima kutoka Tanzania. Yeye ni Mjumbe wa Kamati ya...Mazishi salama na yenye heshima, silaha dhidi ya Ebola nchini DRC
Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mazishi salama na yenye heshima yanaendelea kuwa silaha muhimu katika vita dhidi ya Ebola. Wizara ya Afya ya DRC kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO, na wadau wake, inashirikisha jamii moja kwa moja katika mazishi hayo ili kulinda familia huku mila zikiheshimiwa. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
Shule iliyokuwa ikisomesha mamia ya wanafunzi nchini Haiti sasa ni makazi ya wakimbizi wa ndani 3,000
Shule moja katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, iliyokuwa ikipokea mamia ya wanafunzi, sasa imegeuka kuwa makazi ya muda ya takribani watu 3,000 waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu yenye silaha. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, wakazi hao wanasema maisha katika maskani hayo ni magumu, huku msaada wa kibinadamu ukiwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii
10 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia takwimu za afya barani Afrika, hali ya wakimbizi nchini Haiti, na changamoto za malezi ya watototo wenye ulemavu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), kupitia Ofisi zake za Kanda ya Mashariki ya Mediterania na Afrika, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeandaa Jukwaa la Kwanza la Takwimu za Afya Afrika lililoanza leo Jumanne jijini Nairobi, Kenya. Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye Kituo cha Habari za Umoja wa Mataifa (UNIS) jijini Nairobi, amezungumza na Daktari Hillary Kipruto ambaye ni Afisa Ufundi na Mifumo ya taarifa za Afya kwenye Ofisi ya WHO Kanda ya...Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika laanza Nairobi, Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), kupitia Ofisi zake za Kanda ya Mashariki ya Mediterania na Afrika, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeandaa Jukwaa la Kwanza la Takwimu za Afya Afrika lililoanza leo Jumanne jijini Nairobi, Kenya. Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye Kituo cha Habari za Umoja wa Mataifa (UNIS) jijini Nairobi, amezungumza na Daktari Hillary Kipruto ambaye ni Afisa Ufundi na Mifumo ya taarifa za Afya kwenye Ofisi ya WHO Kanda ya Afrika iliyoko Congo, Brazaville. Daktari Kipruto anaanza kwa kuelezea umuhimu wa takwimu za afya kwani anasema hakuna maendeleo kwenye sekta ya afya b...
Wazazi wa watoto wenye mtindio wa ubongo nchini Kenya wavunja ukimya kuhusu unyanyapaa
Kulea mtoto mwenye changamoto ya kiafya kunaambatana na changamoto nyingi kwa wazazi au walezi. Mbaya zaidi ni pale juu ya changamoto nyingine, wanakumbana na changamoto kubwa zaidi ya unyanyapaa.Nchini Kenya, kupitia ufadhili na mafunzo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake, UN Women, na msaada kutoka kwa familia na jamii, wazazi wa watoto wenye mtindio wa ubongo wameweza kukabiliana na changamoto hizo. Kupitia taarifa hii inayosimuliwa na Augustine Aramba, baadhi ya wazazi wanasimulia kuhusu changamoto hizi na jinsi walivyoweza kukabiliana nazo.
09 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP31, umeanza leo jijini Antalya, Uturuki, ukimulika ajenda mbalimbali ikiwemo ya ufadhili wa hatua za kukabiliana na tabianchi.
Nchini Tanzania, Shirika la Uoja wa Mataofa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa kushirikiana na serikali imetia saini makubaliano ya ruzuku ya dola milioni 2, sawa na shilingi bilioni 5.2, kusaidia taasisi za kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali 49 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Fedha hizo kutoka Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF), kupitia Mpango wa Ruzuku Ndogo (SGP), zinalenga kusaidia miradi ya uhifadhi wa...
06 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Vijana huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania, mashariki mwa bara la Afrika wameshiriki mafunzo ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo endelevu miongoni mwa wanajamii.
Halikadhalika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini humo kwa kushirikiana na wadau wengine wengine wa maendeleo pia yalijikita katika kuwajengea vijana hao uelewa kuhusu Afya ya Akili, usaidizi wa kisaikolojia na kijamii. Rashid Malekela wa UNDP Tanzania amehudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina, kuelekee visiwani Zanzibar kumsikiliza
Pia tunakuleteamuhtasari wa habari:
Mashirika ya Umoja wa Mataifa y...Wanawake nchini Uganda wako mstari wa mbele kutatua migogoro na kujenga amani
Matumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na migogoro ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha amani katika baadhi ya maeneo nchini Uganda. Hata hivyo, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu, huku zaidi ya wapatanishi 1,500 wakipatiwa mafunzo ya kuzuia migogoro na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women kabla haijaongezeka. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu - UNICEF
Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa maelezo zaidi.
05 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia athari za vita kwa upatikanaji wa maji, Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami, na Juhud iza wanawake nchini Uganda za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani..
Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili.Hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa...UNDRR: Ukikumbwa na Tsunami, hatua hizi zitakusaidia kunusurika
Kama nilivyokudokeza hapo awali, hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya Bahari lakini Kamal Kishore, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kupunguza Hatari za Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa au majanga (UNDRR) katika kuadhimisha siku hii, ameeleza hatua tatu muhimu ambazo ukizichukua zinaweza kukuokoa dhidi ya tsunami. Anold Kayanda anatusaidia kueleza kwa lugha ya Kiswahili.
Kutoka kuhofia kuhukumiwa hadi kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya
Zipporah Achieng, mama kijana nchini Kenya, ambaye aliwahi kuhofia kuhukumiwa alipokwenda kliniki kupata huduma za afya baada ya kujifungua, sasa amegeuka kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana. Kupitia mpango wa Together for SRHR, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa kwa lengo hilo la kuelimisha vijana na vijana balehe kuhusu afya ya uzazi, Zipporah anawasaidia vijana kupata taarifa sahihi na huduma za afya ya uzazi bila unyanyapaa. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
Mashambulizi ya droni na uhaba wa mafuta nchini Sudan vyazima matumaini ya raia wanaohitaji msaada wa dharura
Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) yakilenga miundombinu muhimu ya kiraia, ikiwemo vituo vya nishati na mafuta, kuvuruga huduma za afya na maji na kuweka hatarini maisha ya maelfu kwa maelfu ya raia. Flora Nducha anatujuza zaidi
04 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu, hali ya kibinadamu nchini Sudan, na juhudi za wahamasishaji na mashirika ya UN za kuhusu huduma za afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya.
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola.Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya...WHO: Hatua sita za kiafya na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinaweza kuokoa maisha milioni 1.6 kila mwaka
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.
Wakazi wa Lui nchini Sudan Kusini wachoshwa na vita
Wakazi wa Lui, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanalilia amani, elimu na fursa za ajira kwa vijana baada ya kuchoshwa na vita. Kilio hicho kimetolewa wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, walipotembelea eneo hilo kusikiliza changamoto za wananchi kupitia kampeni ya Hear Us, Act Now for Peace yaani Tusikilize, Chukua Hatua sasa kwa ajili ya amani. Cynthia Akhangwa na taarifa zaidi.
Jumuiya ya kimataifa yahimizwa kuisaidia Ukraine wakati huu wa msimu wa baridi
Mcheza filamu maarufu duniani Nikolaj Coster-Waldau anayefahamika zaidi kwa kuigiza katika filamu ya Game of Thrones ambaye pia ni Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani UNDP ametembelea nchini Ukraine kujionea hali ilivyo wakati huu ambao mapigano baina ya Urusi na Ukraine yakiendelea. Leah Mushi anatujuza zaidi kuhusu safari yake hiyo.
03 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC nchini Burundi, Msimu wa baridi kwa waathirika wa vita nchini Ukraine, na juhudi za Umoja wa Mataifan na wakazi wa Sudan kusinini za ujenzi wa amani.
Takriban wakimbizi 125,000 nchini Burundi wako katika hatari ya kukosa msaada wa chakula wa kuokoa maisha kuanzia Januari mwakani, iwapo ufadhili wa dharura hautapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema wakimbizi wengi wamekimbia mzozo wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakitafuta usalama na chakula. Sasa WFP inahitaji dola milioni 40 ili kuendeleza na ku...Wakimbizi 125,000 nchini Burundi hatarini kukosa chakula kuanzia Januari 2027, WFP yaomba msaada wa dharura
Takriban wakimbizi 125,000 nchini Burundi wako katika hatari ya kukosa msaada wa chakula wa kuokoa maisha kuanzia Januari mwakani, iwapo ufadhili wa dharura hautapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema wakimbizi wengi wamekimbia mzozo wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakitafuta usalama na chakula. Sasa WFP inahitaji dola milioni 40 ili kuendeleza na kupanua wigo wa msaada huo. Flora Nducha na ripoti zaidi.
Ethiopia yaandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Timu za Dharura za Matibabu Afrika
Zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi zaidi ya 100 wanatarajiwa kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa kimataifa wa kujadili namna ya kuimarisha uwezo wa nchi kukabiliana na dharura za kiafya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu kwa wakati.Flora Nducha na taarifa zaidi
Umoja wa Mataifa wataka uwajibikaji kwa mauaji kwa wanaowadhuru wanahabari
Ikiwa leo ni siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari duniani hali inaonesha kuzorota na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kukomeshwa vyoto vya ukatili dhidi ya wanahabari na kuhakikisha wanaohusika na mauaji yao wanafikishwa mbele ya sheria, akieleza kuwa mauaji sita kati ya kila saba ya wanahabari duniani hayapati haki. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
02 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari, mifumo ya kukabiliana na dharura za kiafya barani Afrika, na uhamasishaji wa uchunguzi wa mapema ya saratani ya matiti nchini Kenya.
Ikiwa leo ni siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari duniani hali inaonesha kuzorota na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kukomeshwa vyoto vya ukatili dhidi ya wanahabari na kuhakikisha wanaohusika na mauaji yao wanafikishwa mbele ya sheria, akieleza kuwa mauaji sita kati ya kila saba ya wanahabari duniani hayapati haki.Zaidi ya...Kujichunguza matiti kwa dakika chache kunaweza kuokoa maisha - WHO
Je, unajua kuwa unaweza kutumia dakika chache tu kujichunguza matiti yako ukiwa nyumbani? Oktoba ni mwezi wa kimataifa wa kuelimisha umma kuhusu saratani ya matiti na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasisitiza umuhimu wa kutambua dalili, kujichunguza na kupata matibabu kwa wakati. Nchini Kenya, Asha Akinyi Olum kutoka kaunti ya Bungoma ni miongoni mwa wanawake waliofikiwa na huduma za uchunguzi kupitia mpango unaoungwa mkono na WHO. Tupate taarifa Zaidi kutoka kwa Cynthia Akhangwa.
30 OKTOBA 2026
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa hii leo ambapo utasikia muhtasari wa habari na kisha mada kwa kina kutoka Nairobi nchini Kenya ambapo washindi wawili wa tuzo ya Umoja wa Mataifa wamezungumza.
Siku ya Kimataifa ya huduma na usaidizi - ILO yataka uwekezaji katika uchumi wa huduma
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, limetaka hatua za haraka kuchukuliwa kuboresha huduma za malezi na uangalizi, pamoja na mazingira ya kazi kwa watu wanaotoa huduma hizo, likionya kuwa upungufu wa huduma bora unaweza kuongeza ukosefu wa usawa wa kijinsia. Wito huo umetolewa wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, leo tarehe 29 Oktoba. Flora Nducha na taarifa zaidi
UNICEF Tanzania yaimarisha lishe ya watoto kupitia Jiko Darasa Makete
Nchini Tanzania, katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe, mradi wa Lishe ya Mwanao unaowezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF chini ya ufadhili wa Norway umeasaidia kupunguza tatizo la uzito mdogo na udumavu kwa watoto kupitia mafunzo ya upishi wa vyakula vyenye virutubisho vinavyopatikana katika jamii. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
29 OKTOBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, haki za binadamunchini Sudan, na lishe bora kwa watoto kwa lengo la kutokomeza udumavu nchini Tanzania.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, limetaka hatua za haraka kuchukuliwa kuboresha huduma za malezi na uangalizi, pamoja na mazingira ya kazi kwa watu wanaotoa huduma hizo, likionya kuwa upungufu wa huduma bora unaweza kuongeza ukosefu wa usawa wa kijinsia. Wito huo umetolewa wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, leo tarehe 29 Oktoba.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk...Türk aonya kuhusu ukatili dhidi ya raia katika migogoro yanayoendelea duniani
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ukatili dhidi ya raia katika maeneo yenye migogoro duniani, hususan Sudan, ambako mauaji, ubakaji na mashambulizi yanayotumia ndege zisizo na rubani yanaendelea kugharimu maisha ya watu. Aidha amepongeza vijana kwa kusimama kidete kudai haki na uwajibikaji. Leah Mushi ana taarifa zaidi.
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, Mgao au Mwaego
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunamkaribisha NTAHOMBAYE HUSSEIN, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, Mgao au Mwaego.
28 OKTOBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina. Huko DRC ambako mlipuko wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo bado unaendelea, ufuatiliaji wa wagonjwa waliopona ni muhimu kama moja ya sehemu za mwitikio dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huo uliothibitishwa mwezi Mei mwaka huu, ukiwa ni mlipuko wa 17.
Wagonjwa waliopona, mara baada ya kuruhusiwa kwenye vituo vya matibabu, (ETC), huendelea kupatiwa misaada ikiwemo ya kisaikolojia na uchunguzi kupitia kliniki mahsusi.
Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili:
Ripoti mpya ya jarida la kisayansi la Lancet, kwa kushirikiana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Du...