SBS Swahili - SBS Swahili
Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili
Mh Dkt Kosgei"Walemavu hawahitaji huruma, wanahitaji kulindwa kulingana na sheria na katiba ya Kenya"
Mh Dkt Jackson Kosgei ni Askofu mstaafu, na kwa sasa ana hudumu kama mjumbe aliyeteuliwa katika bunge la Kenya.
Taarifa ya Habari:Serikali ya Shirikisho yazingatia hatua zakisheria dhidi ya shirika la OpenAI kwa uvujaji wa taarifa za Medicare
Serikali ya Shirikisho inasema inazingatia hatua za kisheria dhidi ya OpenAI, baada ya mmoja wa mawakala wake kukiuka mfumo wa Medicare wa Australia mnamo Juni, wakati wa tathmini ya ndani ambapo mifumo yake ilikuwa ikitafiti matumizi ya matibabu ya umma.
Albert Mwangi Kuhusu African Australia film fest web
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema Parramatta, kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Noel"ripoti hii ina ushahidi wamambo mazuri tunayo fanya kuliko wanasiasa na vyombo vya habari vinavyo sema"
Shirika la African Australian Advocacy Centre (AAAC), lili zindua ripoti inayo weka wazi michango yawa Australia wenye asili ya Afrika kwa taifa hili usiku wa Jumamosi 19 Septemba 2026.
Dkt Jane "kuna wakati ukienda dukani mlinzi anakufuata fuata, tofauti na wateja wengine ambao si weusi"
Shirika la African Australian Advocacy Centre, lili zindua ripoti inayo weka wazi michango yawa Australia wenye asili ya Afrika kwa taifa hili usiku wa Jumamosi 19 Septemba 2026.
Taarifa ya Habari:Wachumi wasema ripoti ya Serikali kuhusu Vizazi inaonyesha kuwa uchumi utazidi kutegemea ukuaji wa tija katika miongo ijayo
Wanauchumi wanasema kuwa Ripoti ya hivi karibuni ya Serikali kuhusu Vizazi (Intergenerational Report) inaonyesha kuwa uchumi utazidi kutegemea ukuaji wa tija katika miongo ijayo.
Harrison "inabidi tupeleke tamasha hili katika zingine za kanda hili"
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema Parramatta, kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Taarifa ya Habari: Wito watolewa kutokomeza unyanyasaji wa nyumbani nchini Australia
Ripoti mpya kati ya vizazi imetolewa leo, ikionyesha athari za bajeti ya serikali na mitazamo ya uchumi katika miongo minne ijayo.
Naibu Kamishna wa Polisi wa New South Wales Peter McKenna anasema matukio manne tofauti yanayodaiwa kuwa ya unyanyasaji wa nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita yanaonyesha uzito wa janga hilo nchini Australia. Katika tukio lililo ripotiwa katika eneo la Blue Mountains, mvulana wa miaka mitano alikufa, na ndugu zake wawili na mama yake mwenye umri wa miaka 42 walijeruhiwa vibaya baada ya kupatikana na majeraha ya kudungwa visu ndani ya gari katika eneo la Valley Heights.
Kenya...
Yaliyojiri Afrika: Human Rights Watch "Ukosefu wa uchunguzi wa kina na kufunguliwa mashtaka dhidi yawahusika kunaweza endeleza uhalifu nchini Kenya"
Shirika lakutetea haki za binadam la Human Rights Watch lime onya kuwa, makundi ya watu wenye silaha yame endesha mifululizo yamashambulizi dhidi ya mikutano yakisiasa na shughuli za mashirika yakiraia katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.
Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji inayo imarisha sheria kwa wanafunzi wakimataifa na watalii
Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji, ambayo inaimarisha sheria kwa wanafunzi wa kimataifa na watu ambao wako nchini kwa likizo, inalenga wanao baki nchini zaidi ya muda wa viza zao na wanaohama kutoka viza moja hadi nyingine, na inawapa kipaumbele wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta muhimu.
SBS Learn Eng Ep 119 Jinsi yakuzungumza kuhusu mizio ya majani
Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu mizio ya majani?
Makala Leo:Ukandamizaji wa uhamiaji: Labor yaimarisha sheria za viza kwa wanafunzi na watalii
Serikali imefichua mpango wake wa kupunguza uhamiaji halisi wa nje ya nchi hadi watu 225,000 ifikapo 2028, kulingana na utabiri kutoka bajeti ya Mei.
Taarifa ya Habari:Wanafunzi wakimataifa kukabiliwa kwa mkakati wa uhamiaji, wenye sheria kali
Serikali ya shirikisho ime tangaza mabadiliko makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Australia, ikiimarisha sheria kuhusu ni nani anayeweza kuja nchini na ni nani anayeweza baki nchini.
#sbsaudiopodcast
Mh Dkt Kosgei afunguka kuhusu alipoanza kuamani kuwa ulemavu si kutoweza
Mh Dkt Jackson Kosgei ni Askofu mstaafu, na kwa sasa ana hudumu kama mbunge aliyeteuliwa katika bunge la taifa nchini Kenya.
What are Indigenous Protected Areas in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Maeneo Yaliyolindwa yawatu wa Asili nchini Australia ni yapi?
National parks, nature reserves, marine sanctuaries and Indigenous Protected Areas protect different environments and operate under different rules. What makes an Indigenous Protected Area different, and how can you find out whether you are welcome to visit? - Hifadhi za taifa, hifadhi za asili, hifadhi za baharini na Maeneo Yaliyohifadhiwa ya Wenyeji hulinda mazingira tofauti na hufanya kazi chini ya sheria tofauti. Ni nini kinachofanya Eneo Lililohifadhiwa la Wenyeji kuwa tofauti, na unawezaje kujua kama unakaribishwa kupatembelea?
Taarifa ya Habari:Mageuzi ya sheria kuwasilishwa bungeni,kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma
Kifurushi cha mageuzi ya sheria kitawasilishwa katika Bunge la Shirikisho leo, ili kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma, uwekezaji na biashara zinazotumika kuunga mkono mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uvamizi haramu.
Yaliyojiri Afrika:Kamati itakayo fanyia kazi mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar yazinduliwa
Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amezindua Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya vyama vya CCM na ACT-Wazalendo, uteuzi huo wa wajumbe 10 unaashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar.
Prostate cancer in Australia: Testing, treatment and support - Australia Yafafanuliwa:Saratani ya tezi dume nchini Australia: Upimaji, matibabu na usaidizi
About one in five Australian men will be diagnosed with prostate cancer in their lifetime. Understanding the prostate, your risk and the options for testing can help with early detection and treatment. In this episode of Australia Explained, learn about prostate cancer, PSA testing, treatment and support. - Karibu mwanaume mmoja kati ya watano wa Australia atagunduliwa ana saratani ya tezi dume katika maisha yake. Kuelewa tezi dume, hatari yako na chaguzi za kupima kunaweza kusaidia katika kugundua na kutibu mapema. Katika makala haya ya Australia Yafafanuliwa, jifunze kuhusu saratani ya tezi dume, upimaji wa PSA, matibabu na usaidizi.
Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaendelea kukabiliana na shinikizo lakutangaza msimamo wayo kwa viwango vya uhamiaji nchini
Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji.
Makala Leo:Tunachojua kuhusu usalama wakimataifa miaka 25 baada ya tukio la 9/11
Ni miaka 25 tangu karibu watu 3,000 waliuawa katika mashambulizi ya Septemba 11, ambayo yalisababisha Vita dhidi ya Ugaidi vilivyoongozwa na Marekani na kuiingiza Australia katika vita nchini Afghanistan na Iraq.
Mumbi afunguka kuhusu mapokezi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Taarifa ya Habari:Upinzani wa mseto waomba maelezo zaidi kabla ya kura ya mageuzi ya sheria za mitandao ya kijamii zilizo imarishwa
Makampuni ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwapa watumiaji chaguo la kuzima algoriti yao, chini ya rasimu za sheria zilizopangwa kufichuliwa na serikali wiki hii.
Yaliyojiri Afrika:Agizo la Rais Ruto lazua hofu miongoni mwa wahamiaji wenye asili ya Burundi
Nchini Kenya, ukosoaji umekuwa ukiongezeka tangu tangazo la Rais William Ruto Jumatano iliyopita. Alisema kwamba biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wageni nchini Kenya lazima zifunge kuanzia Jumatatu, Septemba 7.
Makala Leo: Unachohitaji kujua kuhusu magonjwa ya msimu huu wa masika
Australia inapo ingia katika majira ya kuchipua, wataalamu wanawasihi watu wasiache kujilinda dhidi ya magonjwa ya msimu.
Taarifa ya Habari:Sera ya malipo ya uzeeni ya One Nation yakosolewa vikali
Chama cha One Nation kina kana kwamba sera yake mpya ya malipo ya uzeeni itasababisha uondoaji mkubwa wa malipo ya uzeeni, au kuongezeka kwa mfumuko wa bei.
Mumbi afunguka kuhusu maandalizi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia
Wanachama wa Jumuiya za Afrika wanao ishi jijini Sydney, New South Wales wana jiandaa kuhudhuria tamasha maalum.
Makala Leo: Dunia yamkumbuka gwiji wa muziki Dolly Parton
Gwiji wa muziki wa Country, Dolly Parton, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.
Yaliyojiri Afrika: CCM yamtimua Dkt Emmanuel Nchimbi
Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM umemvua uanachama Emmanuel Nchimbi na kumpitisha Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kujaza nafasi ya Makamu wa Rais.
Taarifa ya Habari:Australia yatoa kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal
Serikali ya Australia inaanzisha kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal, huku idadi ya Waaustralia waliopotea ikiongezeka hadi 39.
Makala Leo:Kwa nini baraza lamawaziri wakitaifa haliku gusa vituo vya mbadala vya data
Mkutano wa viongozi wa shirikisho, majimbo na wilaya ulimuacha Waziri Mkuu Anthony Albanese akikubali agizo la vituo vya data vinavyoweza kutumika tena.
Makala Leo:Wa Australia 34 miongoni mwa watu ambao wamepotea katika mafuriko Nepal
Takriban watu 160 wameuawa, na mamia wakiwemo watalii na Waaustralia 34 hawajulikani walipo, kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea kwenye mpaka wa Nepal na Tibet.
Taarifa ya Habari:Makumi yawa Australia hawajulikani waliko katika mafuriko nchini Nepal
Waziri Mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa Waaustralia 34, hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa ya ghafla kwenye mpaka wa Nepal-Tibet.
Yaliyojiri Afrika:Ujumbe maalum wafuatilia usitishaji mapigano DRC
Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda.
Taarifa ya Habari:Hospitali za New South Wales kupewa nafasi zaidi za matibabu
Hospitali za New South Wales zitapata nafasi zaidi za matibabu za muda mfupi ili kupunguza shinikizo kwa idara za dharura.
Makala Leo: Mrundikano wa visa za wenza unao waacha waaustralia katika sintofahamu
Mchakato mpya wa kipaumbele ambao unaweza fanya baadhi ya raia wa Australia, wasubiri kwa muda mrefu zaidi kwa wenzi wao kupokea visa umesababisha ukosoaji.
Makala Leo:'Usibofye kitu chochote':Jinsi barua pepe moja inavyoweza haribu biashara
Waaustralia wanapoteza mamia ya mamilioni ya dola kutokana na matapeli, huku matapeli wakizidi kutumia akili mnemba kuwadanganya waathiriwa wao.
Taarifa ya Habari:Ripoti mpya yaitaka Australia iboreshe usalama wa dawa na itoe wakalimani kwa jamii za tamaduni mbalimbali
Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi.
Yaliyojiri Afrika:7 wafariki katika ajali ya helikopta Kenya
Watu saba, wakiwemo raia watano wa Marekani na mkuu wa ujasusi wa Ecuador, wamefariki baada ya helikopta ya watalii kuanguka karibu na Mlima Ololokwe, katika kaunti ya Samburu nchini Kenya.
Makala Leo:Mabadiliko ya NDIS yatakuathiri vipi?
Mamia ya maelfu ya watu watapoteza msaada kutoka NDIS, baada ya mabadiliko yanayolenga kupunguza ukuaji katika mpango huo kupitishwa ndani ya Seneti kwa uungwaji mkono wa Upinzani wa Mseto usiku wakuamkia.
Yaliyojiri Afrika:Askari pori watuhumiwa kwa mauaji ya raia Tanzania
Kituo cha sheria cha haki za binadamu Tanzania, kime eleza wasiwasi kuhusu madai ya watu kuuawa, kujeruhiwa au kupotea katika maeneo ya hifadhi nchini humo.