Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga
Ripoti ya 2025 ya tathmini ya kidunia juu ya kupunguza hatari za majanga inakadiria kuwa gharama kamili ya kukabili majanga ni karibu dola trilioni2.3, na licha ya uwekezaji huu, bajeti za kitaifa bado ni za kiwango cha chini mno.
Vijana walioasi uhalifu na kujitosa katika kutunza mazingira ya kijiji chao
Fahamu kundi la vijana kutoka mtaa wa korogocho jijini Nairobi, walioasi uhalifu na kuamua kutunza mazingira ya jamii yao. Vijana hawa wananuia kuwa mfano kwa kizazi kijacho kufahamu kuwa hata juhudi ndogo zinaweza kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.
Siku ya kimataifa ya hamasisho kuhusu upotevu na uharibifu wa chakula
Wakati mamilioni ya watu wanalala njaa kila siku, chakula kizuri hutupwa mashambani, katika maduka makubwa, mikahawa - na ndiyo, hata katika nyumba zetu wenyewe.
Uharibifu wa chakula sio tu kuhusu kile kilicho kwenye sahani zetu. Pia inahusu rasilimali zinazotumiwa kuzalisha chakula hicho: maji, ardhi, nishati, na raslimali watu, zote hupotea wakati chakula kinaharibika.
ACS2: Addis Ababa: Vijana wasisitiza uwekezaji kwenye ajira za kijani
Uchumi wa kijani ni miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa bara la Afrika uliofanyika hivi majuzi jijini Addis ababa, ambapo wajumbe walijadili mikakati ya kufadhili maendeleo ya kijani barani Afrika kupitia masuluhisho yanayotegemea asili, teknolojia safi.
Mjadala umeibuka kuhusu nafasi ya vijana katika mipango ya serikali za Afrika kuelekea uchumi wa kijani, kupitia ajira za kijani.
Oxfam: Nchi tajiri zimevunja ahadi zao za ufadhili wa hali ya hewa kwa Afrika
Ripoti mpya ya shirika la kimataifa ya Oxfam inasema kuwa nchi tajiri zimetoa tu asilimia 4 pekee ya fedha zinazohitajika Afrika Mashariki kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.
Nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na mzozo wa hali ya hewa, licha ya kuchangia asilimia 0.09 ya uzalishaji wa hewa ukaa duniani.
Wiki ya maji duniani na mabadiliko ya tabianchi: Changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo kame
Vijana Dar es Salaam watumia teknolojia kukabili mafuriko na mabadiliko ya tabianchi
Mtokeo ya majadiliano ya kimataifa kuhusu mkataba wa kisheria wa kukabili taka za plastiki
Kwa mara nyingine tena, dunia ilipoteza fursa muhimu ya kuwa na mkataba huo, majadilianao yakigonga mwamba kutokana na nchi kutofautiana kwenye baadhi ya maandishi.
UN: Ni asilimia 35 pekee ya malengo ya maendeleo endelevu ndio yako katika njia sahihi kufikiwa
Ripoti ya malengo ya maendeleo endelevu mwaka 2025, ikiwa ni miaka kumi tangu mataifa kuanza kufanyia kazi malengo hayo.
Katika ripoti hiyo, UN inasema dunia bado iko nyuma katika kuhakikisha malengo hayo 17 yanaafikiwa kikamilifu kufikia mwaka wa 2030.
Mkataba wa plastiki: Mgawanyiko kuhusu jinsi ya kukabiliana na hatari ya kiafya na kiikolojia.
Mataifa mbalimbali ulimwenguni yameombwa kuchukua hatua na kutatua mzozo wa kimataifa wa plastiki, mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya kiserikali, mwanadiplomasia wa Ecuador, Luis Vayas Valdivieso akiwaomba wadau waliokusanyika Geneva, Uswizi kwa siku 10 kuunda mkataba wa kihistoria wa kuzuia uchafuzi wa plastiki.
"Uchafuzi wa plastiki unaharibu mazingira, unachafua bahari na mito yetu, unatishia viumbe hai, na unadhuru afya ya binadamu," alisema Valdivieso.
Wataalam pia katika ripoti iliyochapishwa kwenye Jarida la matibabu la Lancet, wameonya kuwa uchafuzi wa plastiki ni "hatari kubwa, inayokua na isiyotambulika" kwa afya ambayo inagharimu dunia angalau dola trilioni 1.5 kwa mwaka.
<...Matokeo ya mkutano wa AMCEN katika jitihada za bara la Afrika kukabili mabadiliko ya tabinanchi
Kenya ilikuwa mweneyeji wa mkutano wa 20 wa mawaziri wa mazingira kutoka mataifa ya Afrika, AMCEN, mkutano muhimu kuelekea mikutano ya kimataifa kuhusu mazingira kama vile COP30, INC5.2 na UNEA-7.
Mafanikio ya miaka 50 ya utekelezaji wa CITES, kulinda wanyamapori na mimea
Mkataba wa kimataifa wa CITES ulianza kutekelezwa mnamo Julai mosi 1975. Toka wakati huo mkataba huu umeendelea kusaidia dunia kuzuia kupotea kwa kasi kwa spishi mbalimbali za wanyamapori na mimea zilizokuwa katika hatari ya kutoweka.
Mradi wa EACOP umekamilika asilimia 62, wanaharakati wakiendelea kuupinga
Ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kwenda Tanzania maarufu EACOP umefikia asilimia 62, hivi majuzi raia 26 wa Uganda ambao ni waathriwa wa miradi ya mafuta ya Total ya Tilenga na EACOP wamewasilisha keshi mpya dhidi ya kamuni ya TotalEnergies nchini Ufaransa,
Ziwa Viktoria: Nishati ya sola na biogesi yatoa suluhu ya kukabili taka za mabaki ya samaki na dagaa
Waachuuzi wa samaki na dagaa walilazimika kutumia mbinu za jadi kama vile kuni na makaa kukausha aina hii ya samaki wadogo, dagaa, hali iliyowasababishia hasara na kuchangia uharibifu wa mazingira kwa kutupa taka za samaki ndani ya Ziwa Victoria.
Matumizi ya viuatilifu au viuadudu na madhara kwa mazingira
Hatua ya serikali ya Kenya kuoiga marufuku matumizi ya takriban viuatilifu au dawa za kuua wadudu takriban 77 kutokana na hofu ya usalama wa dawa hizo kwa mazingira na afya ya binadamu.
Baadhi ya viuatilifu vimepigwa marufuku katika soko la kimataifa, kuanzia baranai ulaya, Australia, marekani na Canada, laini viipo kwenye masoko ya nchi za ukanda.
Vitabu: Kampeni ya kuwafikia watoto milioni moja kuhusu uhifadhi
Watoto wana jukumu muhimu katika uhifadhi wa mazingira na wanyamapori kwa kushiriki kikamilifu katika mipango kama vile kupanda miti, udhibiti wa taka, na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mazingira na wanyamapori.
Kuwashirikisha watoto katika shughuli hizi kunakuza hisia ya uwakili, kuwaunganisha na mazingira wanayoishi, na kukuza mazoea endelevu kwa siku zijazo.
Mgogoro wa Bahari: Afrika yataka kushirikishwa kikamilifu katika ulinzi wa bahari
Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kutekeleza lengo nambari 14 la Maendeleo Endelevu, ulifanyika kule Nice, Ufaransa, kujadili mbinu mwafaka za kuhifadhi na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake, washikadau wakiunda uhusiano mpya kati ya wanadamu na mazingira ya baharini.
Mkutano wa kilele ulikamilika Ijumaa tarehe 13 Juni, 2025 wakati huu mataifa yakitarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili sheria za uchimbaji madini kwenye kina kirefu cha maji baharini.
Uhifadhi wa baharini: Hospitali ya kasa Pwani ya Kenya yatoa ahueni kwa viumbe hao
Mataifa yametakiwa kuchukua misimamo mikali kuhusu uvuvi wa kupindukia, uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini.
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Mazingira, taka za plastiki suala kuu
Uchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.
Je dunia iko katika njia sahihi kutimiza lengo la kumaliza njaa kufikia 2030?
Jumatano ya Mei 28 2025, dunia itaadhimisha siku ya njaa ulimwenguni, siku hii ikilenga kutoa hamasa na kuchochea hatua kuchukuliwa ili kumaliza njaa duniani. Kulingana na ripoti ya kimtaifa ya 2025 kuhusu migogoro ya Chakula, zaidi ya watu milioni 295.3 katika nchi 53 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.
Uchakataji wa plastiki katika kuhifadhi mazingira ya bahari na kupata mapato
Jamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.
Mabadiliko ya tabianchi: Hali ya mifumo ya sheria katika kushughulikia ukatili wa kijinsia.
Mabadiliko ya tabianchi yachochea ongezeko la ukatili wa kijinsia
Ripoti hiyo mpya ya UN Spotlight initiative, imebaini kuwa mabadiliko yatabianchi yameendelea kuzidisha mogogoro ya kijamii na kiuchumi ambayo inachochea kuongezeka kwa viwango vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.
Cha kutarajiwa katika ahadi mpya za nchi za kukabili mabadiliko ya tabianchi
Ripoti ya umoja wa mataifa inaonesha dunia ipo nyuma sana katika kudhibiti ongezeko la joto chini ya nyuzi joto 1.5.
Mbolea asilia: Suluhisho kwa uharibifu wa udongo na changamoto za kilimo Kenya
Baadhi ya wakulima nchini Kenya wameanza kugeukia matumizi ya mbolea asilia inayonyunyiziwa ardhini ili kunusuru mashamba yao.
Mabadiliko ya tabianchi yahatarisha barafu ya milimani, barafu hii ikiyeyuka kwa kasi
Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa duniani WMO, barafu inayopatikana kwenye milima inayeyuka kwa kasi zaidi na ndio sababu ya umoja wamataifa kutenga Machi 21 kama siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu kuyeyuka kwa barafu hii.