Neno la Leo
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.
Si Kila “Tuko Sawa” Inamaanisha Tuko Sawa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 14:32–33 tunamwona Absalomu hatimaye akikutana na baba yake, Mfalme Daudi, baada ya miaka mingi ya utengano.
Absalomu anainama mbele ya baba yake na Daudi anambusu.
Kwa macho ya nje, unaweza kusema, “Hatimaye wamepatana!”
Lakini tunapoendelea kusoma simulizi hii, tunagundua kwamba matatizo ya ndani hayakuwa yamekwisha. Baadaye Absalomu anajaribu hata kumpindua baba yake.
Na hapa tunajifunza jambo muhimu:
Kukutana tena sio sawa na kupatanishwa kweli.
Wakati mwingine tunasalimiana, tunakumbatiana na hata kusema “yameisha” lakini bado kuna maumivu, maswali na mambo ambayo ha...
Sio Kila Ukimya Ni Amani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 14:28 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu.
Biblia inatuambia kwamba Absalomu aliishi Yerusalemu kwa miaka miwili bila kuuona uso wa baba yake.
Miaka miwili. Mji mmoja. Baba na mwana. Lakini hakuna mazungumzo.
Na hapa tunajifunza kwamba si kila ukimya ni amani.
Wakati mwingine hatugombani na watu si kwa sababu tumepatana bali kwa sababu hatuzungumzi kabisa.
Tunaweza kuishi nyumba moja, kufanya kazi pamoja au kukutana kila siku lakini mioyo yetu ikawa mbali kwa sababu ya maumivu ambayo hayajashughulikiwa.
War...
Si Kila Anayerudi Amerudishiwa Nafasi Moyoni!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 14:21–24 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu.
Baada ya miaka ya utengano na mipango ya Yoabu, hatimaye Daudi anakubali Absalomu arudi Yerusalemu.
Kwa juu juu, hizi zinaonekana kuwa habari njema.
Mwana anarudi nyumbani.
Lakini kuna jambo la kushangaza.
Daudi anasema:
“Na ageukie nyumbani kwake wala asiuone uso wangu.”
Kwa hiyo Absalomu anarudi Yerusalemu lakini haruhusiwi kukutana na baba yake.
Wako mji mmoja.
Lakini mioyo yao bado iko mbali.
Na hapa tun...
Si Kila Tatizo Jawabu Lake Ni Ukimya!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 14:1–3 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi ambayo imepitia maumivu, ukatili, kisasi na sasa utengano.
Baada ya Absalomu kumuua Amnoni, anakimbia na kuishi mbali na familia yake.
Miaka inapita.
Daudi anamkumbuka mwanawe. Lakini bado hakuna mazungumzo ya kweli yanayoonekana kati yao.
Ndipo Yoabu anatambua hali ya moyo wa mfalme na kupanga njia ya kujaribu kumrudisha Absalomu.
Na hapa tunakutana na ukweli ambao wengi wetu tunaweza kuuhusisha na maisha yetu:
Muda kupita sio sawa na jeraha kupona.
Wakat...
Kisasi Hakiponyi Jeraha!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 13:28–29 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi, ambako maumivu ambayo hayajashughulikiwa sasa yanazaa maumivu mengine.
Jana tulimwona Absalomu akiwa amebeba hasira na chuki dhidi ya Amnoni baada ya kile alichomfanyia dada yake Tamari.
Leo tunagundua jambo muhimu:
Miaka miwili imepita, lakini hasira ya Absalomu haijaisha.
Kwa nje alikuwa kimya. Lakini ndani yake alikuwa amebeba mpango wa kulipiza kisasi.
Hatimaye, Absalomu anaandaa mazingira na kuwaamuru watumishi wake wamuue Amnoni.
Huenda kwa mtazamo wake alikuwa analipiza uovu uliofanywa dhidi ya Tama...
Hatari ya Ukimya!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 13:21–22 tunaendelea na simulizi ngumu ya familia ya Daudi.
Jana tulimwona Tamari akiwa amevunjika baada ya kile Amnoni alichomfanyia.
Leo tunaona kile kinachotokea baada ya familia kujua.
Mfalme Daudi anaposikia habari hiyo anahuzunika sana. Anakereka na kukasirika kwa kile kilichotokea.
Lakini kuna jambo ambalo simulizi linatuacha tukijiuliza:
Baada ya hasira, hatua iko wapi?
Daudi amesikia. Daudi amekasirika. Lakini simulizi halituonyeshi akichukua hatua ya kutosha kushughulikia uovu uliotokea.
Kisha tunamwona Absalomu.
Yeye pia amekasirika. Tamari ni dada...
Usipuuze Maumivu ya Aliyejeruhiwa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 13:19–20 tunabaki katika simulizi ngumu ya Tamari.
Jana tuliona ukatili ambao Amnoni alimfanyia. Leo Biblia haitukimbizi haraka kwenda kwenye tukio jingine.
Inatuonyesha Tamari baada ya tukio.
Anararua vazi lake. Anaweka majivu kichwani. Anaweka mkono kichwani na anaondoka akilia.
Biblia haitufichi maumivu yake.
Na labda nasi hatupaswi kuyakimbia.
Wakati mwingine tunapokutana na mtu aliyeumia, tunakuwa na haraka ya kusema kitu. Tunataka kutoa explanation. Tunataka kumpa advice. Tunataka kumwambia, “Utakuwa sawa.” Au tunataka kupata lesson na kuendelea.
Lakini kuna wakati...
Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka!
🎙️ Leo katika Neno la Leo tunatafakari 2 Samweli 13:10–14, sehemu nzito na yenye maumivu katika simulizi la familia ya Daudi.
Amnoni anapokuwa peke yake na Tamari anajaribu kumlazimisha kutimiza tamaa yake. Tamari anakataa wazi. Anasema, “Usifanye jambo hili.”
Lakini Amnoni hasikilizi.
Anatumia nguvu zake na kumdhuru.
Hapa Biblia inatuweka mbele ya ukweli ambao hatupaswi kuuficha kwa lugha nyepesi:
Tamari alisema hapana. Amnoni hakuheshimu hapana yake.
Huo haukuwa upendo.
Upendo wa kweli haumfanyi mwingine kuwa chombo cha kutimiza tamaa zetu. Upendo haupimi tu kile tunachotaka sisi. Unaheshimu utu, sauti na mi...
Usilishe Tamaa Isiyofaa Moyoni
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 13:1–2 tunaingia katika sehemu ngumu na yenye huzuni katika familia ya Daudi.
Tunamkuta Amnoni akianza kuwa na tamaa isiyofaa kwa Tamari, dada yake wa kambo.
Lakini kuna jambo muhimu ambalo maandiko yanatuonyesha kabla hata hatujafika kwenye kile kitakachotokea baadaye.
Amnoni anaendelea kuibeba na kuilisha tamaa hiyo moyoni mpaka inamtesa.
Na hapa tunahitaji kutofautisha mambo mawili.
Wazo linalopita kichwani na uamuzi wa kulipa nafasi ni vitu viwili tofauti.
Hatuchagui kila wazo linalotokea akilini. Hatuchagui kila temptation inayojitokeza.
Lakini...
Mungu Bado Anaweza Kuandika Sura Mpya!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:24–25 tunafika katika sehemu tofauti kabisa ya simulizi la Daudi.
Tumemwona akikosea vibaya.
Tumemwona akikubali dhambi yake.
Tumemwona akisamehewa lakini akikabiliana na consequences.
Tumemwona akiomba.
Tumemwona akilia.
Na jana tulimwona akiinuka tena.
Leo Biblia inatuonyesha kwamba hadithi haikuishia pale.
Daudi anamfariji Bathsheba. Baadaye wanapata mtoto mwingine:
Sulemani.
Kisha Biblia inasema maneno machache lakini yenye uzito mkubwa:
“Bwana akampenda.”
Hapa tunahitaji kuwa careful tusikimbilie kuifanya sehemu hii kana kwamba...
Baada ya Siku Ngumu, Unaweza Kuinuka Tena
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:20 tunakutana na Daudi baada ya kupokea jibu ambalo hakulitaka.
Jana tulimwona akiwa chini, akifunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto wake.
Leo habari inafika:
Mtoto amekufa.
Watumishi wa Daudi wanaogopa hata kumwambia. Wanafikiri kama alikuwa katika hali ile mtoto akiwa hai, atakuwaje akigundua kwamba amekufa?
Lakini Daudi anaposikia habari hiyo anafanya jambo ambalo hawakutarajia.
Anaondoka chini. Anaoga. Anabadilisha mavazi. Anaingia katika nyumba ya Bwana na kuabudu.
Hii haimaanishi Daudi hakuhuzunika.
Haimaanishi kilichotokea hakik...
Omba Hata Kama Hujui Mungu Atajibu Vipi!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:16–17 tunamwona Daudi katika sehemu tofauti kabisa na jana.
Jana alisimama mbele ya Nathani na kukubali:
“Nimemkosea Bwana.”
Leo yuko chini mbele za Mungu akiomba.
Mtoto wake anaumwa sana. Daudi anafunga, anaingia ndani na kulala chini usiku kucha akimtafuta Mungu.
Na hapa kuna jambo la kuvutia.
Daudi tayari amesikia kile Nathani alichosema. Hajui kama hali itabadilika.
Lakini bado anaomba.
Hapo tunajifunza jambo muhimu kuhusu maombi.
Wakati mwingine tunaingia katika maombi tukijua kabisa tunachotama...
Ukikosea, Usijifiche. Rudi kwa Mungu!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 12:13–14 tunakutana na moja ya moments nzito zaidi katika maisha ya Daudi.
Nabii Nathani amesimama mbele yake na kumwambia wazi:
“Wewe ndiye mtu huyo.”
Daudi sasa hana mahali pa kujificha.
Angeweza kujitetea. Angeweza kutoa sababu. Angeweza kutumia mamlaka yake kama mfalme kumyamazisha Nathani.
Lakini Daudi anasema:
“Nimemkosea Bwana.”
Hakuna excuse. Hakuna blame shifting.
Anakubali.
Na Nathani anamjibu kwamba Bwana ameiondoa dhambi yake.
Hapo tunaona uzuri mkubwa wa neema ya Mungu.
Baada ya y...
Maliza Vizuri!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 30:23–26 na 31:1–4 tunafunga mwezi wetu na wakati huohuo tunafika mwisho wa safari yetu kupitia kitabu cha 1 Samweli.
Na Biblia inatuacha na picha mbili tofauti sana:
Daudi na Sauli.
Daudi anatoka katika kipindi kigumu sana kule Ziklagi. Ameona mji wake ukiteketea. Amelia mpaka hana nguvu. Watu wake wametaka kumpiga mawe.
Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, akamwuliza Mungu hatua inayofuata na mwisho akapata ushindi.
Baada ya ushindi, baadhi ya watu wake wanataka kujichukulia nyara na kuwanyima wale waliokuwa wamechoka na kubaki nyuma.
Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulichofikiri Kimepotea!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 30:8, 18–19 tunaendelea na Daudi baada ya moja ya siku ngumu zaidi katika maisha yake.
Jana tulimwacha Ziklagi ikiwa imechomwa moto. Familia zimechukuliwa mateka. Watu wake wamevunjika moyo kiasi cha kutaka kumpiga mawe.
Daudi akalia mpaka hakuwa na nguvu tena za kulia.
Lakini Biblia ikasema:
“Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake.”
Leo tunaona jambo muhimu sana. Baada ya kupata nguvu, Daudi hafanyi maamuzi kwa hasira. Hakimbilii kuwafukuza Waamaleki kwa sababu tu anajua kupigana.
Anafanya kitu ambacho tumemwona akikifanya kabla:
<...Unaweza Kulia na Bado Ukawa na Imani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 30:3–6 tunakutana na moja ya siku nzito zaidi katika maisha ya Daudi.
Daudi na watu wake wanarudi Ziklagi wakitarajia kurudi nyumbani. Lakini wanapofika, wanakuta mji umechomwa moto na familia zao zimechukuliwa mateka.
Biblia inasema:
“Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao wakalia hata walipokuwa hawana nguvu tena za kulia.”
Hawa ni mashujaa.
Wamepitia vita. Wameishi jangwani. Wamekabiliana na hatari nyingi.
Lakini leo wanalia.
Na Daudi analia pamoja nao.
Huyu ni Daudi aliyesimama mbele ya Go...
Usifanye Maamuzi Makubwa Ukiwa Umechoka na Kuogopa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 27:1 tunakutana na Daudi katika hali ambayo huenda wengi wetu tunaifahamu.
Jana alikuwa amesimama imara katika imani. Alikuwa na nafasi nyingine ya kumuua Sauli lakini akakataa. Alikuwa tayari kumwachia Mungu matokeo.
Lakini leo tunamsikia Daudi akisema moyoni mwake:
“Siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli.”
Ngoja kidogo.
Huyu si Daudi aliyemshinda Goliathi? Si huyu ambaye Mungu amemwokoa kutoka kwa Sauli tena na tena? Si huyu ambaye tayari amepakwa mafuta kwa ajili ya kusudi kubwa?
Ndiyo.
Lakini Daudi ame...
Usijilipizie Kisasi Hata Ukipewa Nafasi
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 26:9–11 tunamwona Daudi akikabiliwa tena na mtihani ambao tayari aliwahi kuupita.
Mara ya kwanza Sauli aliingia katika pango ambamo Daudi alikuwa amejificha. Daudi alikuwa na nafasi ya kumuua lakini akakataa.
Sasa inatokea tena.
Daudi na Abishai wanaingia kambini usiku na kumkuta Sauli amelala. Mkuki wake uko karibu na kichwa chake. Abishai anaangalia mazingira na anafikia conclusion ambayo wengi wetu tungeweza kufikia: “Mungu amemtia adui yako mikononi mwako.”
Fikiria kama ungekuwa Daudi. Mara ya kwanza pangoni. Sasa mara ya pili kambini.
Angeweza ku...
Si Kila Anayekuzuia Ni Adui Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 25:32–33 tunakutana na jambo la kushangaza kuhusu Daudi.
Jana tulimwona akikataa kulipiza kisasi kwa Sauli. Lakini leo Daudi mwenyewe anakaribia kufanya kile alichokataa kufanya jana.
Nabali amemdharau na Daudi amekasirika. Anaondoka akiwa tayari kulipiza kisasi.
Ndipo Abigaili anapoingia katika simulizi.
Anamfuata Daudi na kuzungumza naye kwa hekima. Anamzuia. Anamfanya afikirie tena kabla hasira haijampeleka kwenye uamuzi ambao angekuja kujutia.
Na baada ya kumsikiliza, Daudi anatambua jambo kubwa. Anasema kwa maana, “Na ahimidiwe Bwana aliyekutuma… umenizuia nisiingie katika hatia.”
Hii inatufund...
Usiruhusu Aliyekuumiza Abadilishe Wewe Ni Nani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Kupitia 1 Samweli 24:12 tunaendelea na Daudi baada ya kukataa kumuua Sauli pangoni.
Daudi anatoka nje na kumwonyesha Sauli kipande cha vazi lake. Ujumbe ni wazi: “Nilikuwa na nafasi ya kukuua, lakini sikufanya hivyo.”
Kisha anasema, “Bwana na ahukumu kati yangu na wewe… lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.”
Daudi hakujifanya kwamba Sauli hajamkosea. Sauli alikuwa amemfanyia mabaya. Alikuwa amemfukuza, ametishia maisha yake na kumfanya aishi kama mkimbizi.
Lakini Daudi anakataa jambo moja: hatamruhusu Sauli aamue Daudi atakuwa mtu wa aina gani.
Na hapo ndipo kuna somo...
Si Kila Mlango Uliofunguka Ni Mlango wa Mungu!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Kupitia 1 Samweli 24:4–6 tunamwona Daudi akikabiliwa na nafasi ambayo kwa macho ya kibinadamu inaonekana kama jibu la maombi yake.
Sauli amekuwa akimtafuta ili kumuua. Lakini sasa, bila kujua, Sauli anaingia katika pango lilelile ambamo Daudi na watu wake wamejificha.
Watu wa Daudi wanaona jambo moja tu: “Hii ndiyo nafasi yako!” Adui yako yuko mbele yako. Hakuna anayekuzuia. Unaweza kumaliza tatizo lako leo.
Lakini Daudi anatambua jambo muhimu: kuwa na nafasi ya kufanya kitu hakumaanishi una ruhusa ya Mungu kukifanya.
Na sisi tunaweza kuingia katika mtego huo. Mlango...
Kuwa Mtu Anayeimarisha Imani ya Wengine
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:16 tunakutana tena na Yonathani. Daudi bado anakimbia. Sauli bado anataka kumuua na mazingira yake bado hayajabadilika.
Lakini Yonathani anamtafuta Daudi.
Na Biblia haisemi tu kwamba alikuja kumtembelea au kumfariji. Inasema jambo zuri sana:
“Akamwimarisha mkono wake katika Mungu.”
Yonathani hakuondoa Sauli. Hakutatua tatizo la Daudi. Hakumwahidi kwamba kesho kila kitu kitakuwa sawa. Alifanya jambo ambalo angeweza kufanya: alimsaidia Daudi kumwangalia Mungu tena.
Huyo ni rafiki wa thamani.
Kuna wakati mtu anayepitia kipindi kigumu hahitaji wewe uwe na majibu yo...
Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:14 tunamkuta Daudi bado anakimbia. Sauli hajakata tamaa. Maandiko yanasema alikuwa akimtafuta Daudi kila siku.
Lakini katikati ya simulizi hiyo kuna maneno machache yenye ujumbe mkubwa sana:
“Lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.”
Angalia jambo hilo. Mungu hakumwondoa Sauli mara moja. Hakumaliza tatizo lote siku hiyo. Daudi bado alikuwa jangwani. Bado alikuwa anahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Bado kulikuwa na hatari na uncertainty.
Lakini Mungu alikuwa anamshikilia katikati ya hayo yote.
Mara nyingi tunafikiri ulinzi wa Mungu lazima uonekane kwa tatizo ku...
Muulize Mungu Kabla ya Kuchukua Hatua!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:2 tunamwona Daudi akikabiliwa na uamuzi mwingine muhimu. Anaambiwa kwamba Wafilisti wanashambulia Keila na kuiba mazao yao.
Daudi alikuwa na sababu nyingi za kujiamini. Huyu ndiye aliyemshinda Goliathi. Ana uzoefu wa vita. Sasa ana watu wanaomfuata. Angeweza kusikia taarifa hiyo na kusema, “Hili nalijua. Twendeni kupigana.”
Lakini jambo la kwanza Daudi anafanya linatufundisha kitu muhimu sana:
“Daudi akauliza kwa Bwana.”
Daudi alikuwa na uwezo lakini hakuruhusu uwezo wake uchukue nafasi ya mwongozo wa Mungu.
Na hapo ndipo Neno la leo linapotufikia...
Usihitimishe Hadithi Yako Ukiwa Pangoni!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 22:1–2 tunamkuta Daudi mahali ambapo huenda hakuwahi kufikiria angefika: katika pango la Adulamu.
Fikiria safari yake. Alipakwa mafuta kuwa mfalme. Akamshinda Goliathi. Wanawake wakaimba jina lake. Akaingia katika nyumba ya mfalme na kila kitu kikaonekana kinaelekea juu.
Lakini sasa yuko pangoni.
Kwa macho ya kawaida, unaweza kuangalia maisha ya Daudi na kusema, “Kuna kitu kimeharibika.” Aliyeahidiwa ufalme anawezaje kuwa mkimbizi pangoni?
Lakini Mungu bado hajamaliza.
Akiwa katika pango hilo, watu wanaanza kuja kwa Daudi. Wenye dhiki, wenye madeni na wenye uchungu wa...
Hata Watu wa Imani Huogopa!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 21:12–13 tunakutana na upande tofauti kabisa wa Daudi.
Huyu ndiye Daudi aliyesimama mbele ya Goliathi wakati jeshi lote la Israeli limejaa hofu. Huyu ndiye aliyesema, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Huyu ndiye aliyetangaza, “Vita ni vya Bwana.”
Lakini leo Biblia inatuambia kwamba Daudi akaogopa sana.
Akiwa anakimbia kutoka kwa Sauli, anafika Gathi na anapotambua hatari aliyomo, hofu inamjaa kiasi kwamba anajifanya mwendawazimu ili kuokoa maisha yake.
Huyu bado ni Daudi.
Na hilo linatufundisha jambo muhimu sana: kuwa na imani hakumaanishi kwamba hutawahi...
Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia?
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 20:17 tunaendelea kuangalia urafiki wa ajabu kati ya Daudi na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba Yonathani alimpenda Daudi kama alivyoipenda nafsi yake mwenyewe na akamtaka athibitishe tena kiapo chao.
Lakini kuna kitu kinachoufanya urafiki huu kuwa wa kipekee zaidi.
Yonathani alikuwa mwana wa mfalme. Kwa kawaida angeweza kutarajia kwamba siku moja angechukua nafasi ya baba yake. Lakini kadiri Daudi anavyosogea katika kusudi la Mungu juu ya maisha yake, ndivyo uwezekano wa Yonathani kuwa mfalme unavyopungua.
Yonathani angeweza kumwangalia Daudi na kuona competitor. Badala yake, alimwona rafik...
Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 19:4–5 tunamwona Yonathani akifanya jambo linalotuonyesha maana nyingine ya urafiki wa kweli.
Sauli sasa anataka Daudi auawe. Daudi hayupo kwenye mazungumzo haya lakini Yonathani yupo. Na badala ya kukaa kimya, anamkumbusha baba yake ukweli: Daudi hajamkosea. Anamkumbusha jinsi Daudi alivyohatarisha maisha yake kupigana na Goliathi na jinsi Mungu alivyotumia ushindi wake kuleta furaha kwa Israeli.
Lakini kuna jambo kubwa zaidi hapa. Yonathani angeweza kufaidika Daudi akiondolewa. Kama mwana wa Sauli, alikuwa na maslahi yake mwenyewe katika kiti cha enzi. Hata hivyo, Yonathani anachagua kilicho sahihi kuliko kile ki...
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”
Ni rahisi kusimama kwenye sehemu ya kwanza, “Daudi akafanikiwa.” Lakini siri ya maisha yake ipo katika sehemu inayofuata: “Bwana alikuwa pamoja naye.”
Mwezi huu tumemfuata Daudi kutoka malishoni. Tulimwona akiwa kijana asiyepewa nafasi kubwa hata ndani ya familia yake. Akaingia ikulu. Akasimama mbele ya Goliathi. Akapata ushindi na jina lake likaanza kujulikana katika Israeli. Sasa Sauli anaanza kumwonea wivu na kumwangalia kwa mashaka.
<...Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:7–9 tunaona mabadiliko ya kusikitisha yakianza ndani ya moyo wa Sauli. Baada ya ushindi, wanawake wanaimba wakisema Sauli amewaua maelfu yake na Daudi makumi ya maelfu yake. Sauli anasikia comparison hiyo na kuanzia hapo anaanza kumwangalia Daudi kwa jicho tofauti.
Lakini Daudi hajamkosea Sauli. Tatizo ni kwamba mafanikio ya Daudi yameanza kumfanya Sauli ajisikie mdogo.
Na hapo ndipo wivu huanzia mara nyingi. Mtu mwingine anapata promotion na badala ya kufurahi tunaanza kujiuliza, “Kwa nini si mimi?” Biashara yake inakua. Anaolewa au anaoa. Anapata mtoto. Ananunua nyumba. Anapata naf...
Mungu Hutupa Watu wa Kutembea Nasi!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 18:1–3 tunaanza kuona maisha ya Daudi baada ya ushindi dhidi ya Goliathi. Lakini jambo la kwanza tunalokutana nalo si vita nyingine. Tunakutana na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba moyo wa Yonathani uliungana na moyo wa Daudi, akampenda kama nafsi yake mwenyewe na wakafanya agano la urafiki.
Kwa wakati huu Daudi huenda hajui umuhimu ambao urafiki huu utakuwa nao. Siku zinazokuja hazitakuwa rahisi. Sauli ataanza kumwonea wivu, Daudi atafukuzwa na wakati mwingine maisha yake yatakuwa hatarini. Na katika kipindi hicho, Yonathani atakuwa mmoja wa watu muhimu sana katika maisha yake.
Mu...
Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:49–50 tunafika katika wakati ambao tumekuwa tukiuelekea kwa siku kadhaa. Daudi anaweka mkono katika mfuko wake, anachukua jiwe, analitia katika kombeo na kumpiga Goliathi kwenye paji la uso. Yule mtu aliyekuwa amelitia hofu jeshi zima la Israeli anaanguka.
Goliathi alikuwa na upanga, mkuki, deraya na uzoefu mkubwa wa vita. Daudi alikuwa na kombeo na jiwe.
Lakini tayari tumejifunza kwamba nguvu ya Daudi haikuwa katika jiwe. Tumaini lake lilikuwa kwa Bwana. Hata hivyo, Mungu hakumwambia Daudi atupe kombeo lake. Daudi alimtegemea Mungu huku akitumia kile ambacho tayari alikuwa...
Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.”
Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo lake.
Kwa hiyo kusema “vita ni vya Bwana” hakumaanishi kwamba hatuna sehemu ya kufanya. Inamaanisha tunajua tofauti kati ya wajibu wetu na kile ambacho ni Mungu pekee anaweza kufanya.
Na hapo ndipo Neno la leo linap...
Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.”
Lakini angalia jambo hili. Baada ya kusema vita ni vya Bwana, Daudi hakukaa chini akisubiri Mungu afanye kila kitu. Bado alikimbia kuelekea kwa Goliathi. Bado alichukua jiwe. Bado alitumia kombeo lake.
Kwa hiyo kusema “vita ni vya Bwana” hakumaanishi kwamba hatuna sehemu ya kufanya. Inamaanisha tunajua tofauti kati ya wajibu wetu na kile ambacho ni Mungu pekee anaweza kufanya.
Na hapo ndipo Neno la leo linap...
Kwa Jina la Bwana!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa vita na mwonekano wa kutisha. Daudi ana fimbo, kombeo na mawe.
Kwa macho ya kibinadamu, hakuna ushindani.
Lakini Daudi anasema: “Wewe unanijia kwa upanga na fumo na mkuki, bali mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa majeshi.”
Na hapo ndipo tunagundua siri ya ujasiri wa Daudi.
Haikuwa kombeo. Haikuwa jiwe. Wala haikuwa confidence kubwa ndani yake mwen...
Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:38–40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na kumpa upanga. Ni vifaa vizuri kabisa vya vita, lakini Daudi anapojaribu kutembea navyo anatambua jambo muhimu: hajavizoea.
Anavivua.
Badala yake anachukua fimbo yake, mawe matano laini na kombeo lake, vitu ambavyo alikuwa amejifunza kuvitumia muda mrefu akiwa malishoni.
Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila kitu kinachomfaa mtu mwingine kitakufaa wewe. Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu, kupokea ushauri, mentors...
Kumbuka Mungu Alivyokusaidia Zamani!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:34–37 tunagundua siri ya ujasiri ambao Daudi alionyesha jana. Sauli anamwangalia Daudi na kuona kijana asiye na uzoefu wa vita. Goliathi, kwa upande mwingine, amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake. Kwa macho ya Sauli, Daudi hana kile kinachohitajika.
Lakini Daudi anajua jambo ambalo Sauli halijui. Ana historia na Mungu.
Anamweleza jinsi alipokuwa akichunga kondoo wa baba yake na simba au dubu akaja kuchukua kondoo, Daudi alimfuata na kumwokoa. Kisha anasema kwa ujasiri: Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba na dubu ataniokoa pia na mkono wa huyu Mf...
Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:32 tunafunga wiki yetu ya kwanza ya Septemba tukiwa tumemfuata Daudi kutoka malishoni mpaka sasa amesimama mbele ya mfalme.
Kwa siku nyingi jeshi la Israeli limekuwa likimsikiliza Goliathi akitoa vitisho. Kila anapotokea, hofu inaenea. Wanaume waliofunzwa vita wanaona ukubwa wa tatizo na mioyo yao inakata tamaa. Lakini Daudi, kijana ambaye hata hakuwa mwanajeshi, anafika mbele ya Sauli na kusema, “Moyo wa mtu yeyote usizimie kwa ajili yake. Mtumishi wako atakwenda kupigana na huyu Mfilisti.”
Mazingira hayajabadilika. Goliathi bado yupo. Jeshi la Wafilisti bado lipo. Kilichobadilika ni kwamba sa...
Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako!
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:28–29 tunaendelea na simulizi ya Daudi na Goliathi. Jana tuliona Daudi akiitazama changamoto kwa macho tofauti. Lakini kabla hajafika hata mbele ya Goliathi, anakutana na vita nyingine ambayo huenda hakuitarajia: maneno ya ndugu yake mwenyewe, Eliabu.
Eliabu anamsikia Daudi akiuliza kuhusu Goliathi, anakasirika na kuanza kumshutumu. Anahoji sababu ya Daudi kuja vitani na hata kutafsiri vibaya nia ya moyo wake.
Fikiria hilo: Daudi hajapigana na Goliathi lakini tayari kuna mtu anayemwambia, kwa namna fulani, “Wewe unafanya nini hapa?”
Na maisha yanaweza kuwa hivyo pia. Kabla hujaf...
Usimfanye Goliathi Wako Kuwa Mkubwa Kuliko Mungu
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 17:26 tunaingia katika moja ya simulizi zinazojulikana zaidi katika Biblia, simulizi ya Daudi na Goliathi. Lakini kabla Daudi hajachukua jiwe, kabla hajatumia kombeo na kabla Goliathi hajaanguka, kuna jambo muhimu sana linalotokea: Daudi anaiona hali ileile ambayo kila mtu anaiona lakini anaichukulia kwa mtazamo tofauti.
Jeshi lote la Israeli lilimwona Goliathi. Waliona ukubwa wake, silaha zake na hatari aliyokuwa nayo. Daudi naye aliona mambo hayo. Imani yake haikumfanya ajifanye kwamba Goliathi hayupo au kwamba si hatari.
Tofauti ilikuwa hii: wengine walimwangalia Goliathi wakajilinganisha naye. Daudi alimwangalia Golia...